logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wakaazi washuhudia kisanga mti ulioanguka na kukauka miaka 7 iliyopita kunuka tena

Mti upo katika bustani ya mkulima mmoja kwa jina Enock Mukalazi,

image
na Radio Jambo

Habari29 November 2023 - 07:07

Muhtasari


• Kwa mujibu wa Nile Post, Wakaazi kutoka vijiji tofauti walikusanyika kushuhudia mti huu ulioinuka bila msaada wa mtu yeyote.

Mti ulioanguka.

Wakazi wa Kijiji cha Busagula katika Halmashauri ya Mji wa Kigangazi, Wilaya ya Bukomansimbi nchini Uganda walishuhudia kisanga cha taharuki baada ya mti ulioanguka miaka saba iliyopita kuinuka.

Kwa mujibu wa Nile Post, Wakaazi kutoka vijiji tofauti walikusanyika kushuhudia mti huu ulioinuka bila msaada wa mtu yeyote.

Wenyeji walisimulia kuwa mti huo, ulikua kwa miaka 30 baada ya kupandwa lakini mnamo 2016 mvua kubwa iliuangusha.

Walakini, wiki hii walishangaa baada ya mti kuinuka.

“Wote ilianguka chini hata mizizi ilikuwa nje ya ardhi. ”

Mti upo katika bustani ya mkulima mmoja kwa jina Enock Mukalazi, mkazi wa Busagula, katika Halmashauri ya Mji wa Kigangazi Wilaya ya Bukomansimbi.

Wakazi waliambia jarida hilo kuwa mti huo uliwashangaza kulingana na mwonekano wake.

"Wiki iliyopita nilichota kuni kutoka kwa mti huu wa Mutuba na nimekuwa nikiokota kuni kutoka kwake lakini nilishangaa nilipoambiwa kuwa uliinuka," Tusasirwa Florence mkazi wa kijiji cha Busagula alisema.

Baadhi ya wakazi hao wameona hii ni baraka kutoka kwa Mungu na wengine wameanza kuweka sarafu na mbegu za kahawa chini ya mti huku wakipiga magoti kuomba baraka kutoka kwa mababu zao.

Wakazi hao walisema kuwa hii si mara ya kwanza kuona maajabu hayo kijijini kwao bali wanauliza kwa nini huwa ni wao kila mara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved