Wafungwa wa Urusi waliokuwa wakiachiliwa baada ya miezi 6 sasa 'kupigana hadi kufa'

Awali ulikuwa unaweza kupigana kwa miezi sita halafu uanapewa msamaha. Lakini sasa, unalazimika kupigana hadi mwisho wa vita,

Muhtasari

•Wafungwa hawapati tena msamaha, wanakabiliwa na hali ngumu zaidi na badala ya kurudi nyumbani mapema, lazima wapigane hadi mwisho wa vita.

Image: BBC

Urusi imekuwa ikiwaachilia wafungwa kupigana nchini Ukraine kwa zaidi ya mwaka mmoja, awali ikiwapa msamaha na uhuru baada ya miezi sita, hata kama wamepatikana na hatia ya uhalifu wa kutumia nguvu.

Lakini BBC imegundua mpango huu ni kitu cha zamani. Sasa, hawapati tena msamaha, wanakabiliwa na hali ngumu zaidi na badala ya kurudi nyumbani mapema, lazima wapigane hadi mwisho wa vita.

"Ikiwa utajiandikisha sasa, uwe tayari kufa," anaandika mtu anayeitwa Sergei kwenye chumba cha mazungumzo cha wafungwa wa zamani wa Urusi wanaopigana huko Ukraine.Anasema kuwa tangu Oktoba amekuwa sehemu ya aina mpya ya kitengo cha jeshi kwa jina "Storm V" ambacho wafungwa sasa wanapewa."

Awali ulikuwa unaweza kupigana kwa miezi sita halafu uanapewa msamaha. Lakini sasa, unalazimika kupigana hadi mwisho wa vita," anaandika.

Wakati usajili wa wafungwa wengi Urusi ulipoanza katika msimu wa joto wa 2022, uliongozwa na Yevgeny Prigozhin, aliyekuwa mkuu wa kikundi cha kijeshi cha kibinafsi cha Wagner. Wafungwa walipewa rekodi safi, msamaha kamili na kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya miezi sita kwenye uwanja wa vita.

Kabla ya kufariki katika ajali ya ndege mwezi Agosti, Prigozhin alisema kuwa karibu wafungwa 50,000 wa Urusi walikuwa wametumwa mstari wa mbele chini ya mkataba huu - takwimu kama hizo zimetajwa na wanaharakati wa haki za binadamu.

Maelfu ya wafungwa hao walikufa, lakini wengine, walimaliza miezi sita na kurudi nyumbani na wengine waliendelea kufanya makosa tena na hata kuua.Jeshi la Urusi lilichukua mpango huo mnamo Februari 2023, hapo awali likitoa motisha sawa na Prigozhin.

Lakini mpango huo ulimaanisha kuwa wafungwa walioachiliwa kupigana wangeweza kurudi nyumbani baada ya miezi sita na walikuwa katika nafasi ya upendeleo kuliko wanajeshi wa kawaida.

Jambo hilo liliwakasirisha wanaume ambao walikuwa wamehamasishwa na familia zao.Sasa, masharti mapya kwa wafungwa yanarekebisha usawa huo na ni magumu zaidi.