Kiongozi wa upinzani nchini Chad ameuawa wakati wa majibizano ya risasi na vikosi vya usalama, mwendesha mashtaka wa serikali anasema.
Kifo cha Yaya Dillo kinakuja baada ya serikali kulaumu chama chake cha upinzani kwa shambulio baya dhidi ya shirika la usalama la nchi hiyo, ambalo Bw Dillo alikanusha.
Siku ya Jumatano, milio ya risasi ilisikika karibu na makao makuu ya chama chake katika mji mkuu.
Mwendesha mashtaka Oumar Mahamat Kedelaye alithibitisha kifo cha Bw Dillo mnamo Alhamisi.