Mwanaume 'apata afueni kubwa' baada ya kupandikizwa figo ya nguruwe

Madaktari wa upasuaji wanasema Rick Slayman ni "shujaa halisi" kwa kuwa wa kwanza kujaribu upasuaji huo.

Muhtasari

•Mzee huyo alipata figo mpya kutoka kwa nguruwe ambayo ilibadilishwa vinasaba ili kupunguza hatari ya kukataliwa kwa kiungo hicho.

Image: BBC

Mzee wa miaka 62 anasemekana kupata nafuu na anatakiwa kuondoka hospitalini hivi karibuni, baada ya kupata figo mpya kutoka kwa nguruwe ambayo ilibadilishwa vinasaba ili kupunguza hatari ya kukataliwa kwa kiungo hicho.

Madaktari wa upasuaji wa Marekani wanasema Rick Slayman ni "shujaa halisi" kwa kuwa wa kwanza kujaribu upasuaji huo.

Lengo la mwisho ni kutumia viungo vya wanyama kwa upandikizaji zaidi.

Siku za nyuma, figo za nguruwe ziliwekwa ndani ya ubongo watu waliokufa kwa kama majaribio.

Upasuaji huo wa saa nne, uliofanyika tarehe 16 Machi, "unaashiria hatua kubwa katika jitihada za upatikanaji wa viungo vinavyopatikana kwa urahisi zaidi kwa wagonjwa", Hospitali Kuu ya Massachusetts ilisema katika taarifa.

Bw Slayman alipandikizwa figo ya binadamu katika hospitali hiyo hiyo mwaka wa 2018 baada ya kuwa kwenye matibabu kwa miaka saba kwa sababu figo zake mwenyewe hazikuwa zikifanya kazi ipasavyo.