Mchezaji wa zamani wa Chelsea amtema mkewe baada ya kugundua si baba mzazi wa watoto wake

Uchunguzi wa DNA ulifichua kuwa baba mzazi wa watoto hao mapacha alikuwa mume wa zamani wa mkewe.

Muhtasari

•Geremi Njitap ameomba talaka kutoka kwa mkewe, Laure Fotso baada ya kubaini kuwa yeye si baba mzazi wa watoto wake.

•Katika karatasi za mahakama, Geremi alisema mkewe aliharibu maelewano ya ndoa yao kupitia tabia yake mbaya.

walikuwa wachezaji wenzake Chelsea
Geremi Njitap na Didier Drogba walikuwa wachezaji wenzake Chelsea
Image: HISANI

Kiungo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Geremi Njitap ameomba talaka kutoka kwa mkewe, Laure Fotso baada ya kubaini kuwa yeye si baba mzazi wa watoto wake.

Geremi, 45, aliamua kuwasilisha talaka mahakamani baada ya uchunguzi wa DNA kufichua kuwa baba mzazi wa watoto hao mapacha alikuwa mume wa zamani wa mkewe.

Mke wa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Bi Laure alidaiwa kushiriki uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake wa zamani alipokuwa naye.

Hadi uchunguzi wa DNA ulipofika, mwanasoka huyo wa zamani aliamini watoto hao mapacha ni wake.

Katika karatasi za mahakama, Geremi alisema mkewe aliharibu maelewano ya ndoa yao kupitia tabia yake mbaya.

Hati za mahakama pia zinataja uwongo wa mara kwa mara wa Laure, na kuongeza: "Hakuna watoto ambao wamezaliwa kutoka kwa muungano huu.”

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, mke wa Jeremi alidai kwamba mapacha hao waliozaliwa Juni 2008,  na ambao wana miaka minne kabla ya ndoa yao walikuwa wa mchezaji huyo wa zamani, jambo lililowachochea kuoana.

"Lakini ugunduzi kwamba watoto hao walikuwa wa mwenzi wake wa awali uliharibu maelewano ya wenzi hao. Ilimletea mshtuko mkubwa wa kihemko,” stakabadhi za mahakama zilisema.

Geremi alicheza mechi 109 akiwa Chelsea kati ya 2003 na 2007, akifunga mabao manne.

Aliichezea Real Madrid kati ya 1999 na 2003.

Katika ulingo wa kimataifa, alikuwa sehemu ya timu ya Cameroon iliyorekodi ushindi mtawalia wa AFCON mnamo 2000 na 2002.