Tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi katika miaka 25 laikumba Taiwan

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 katika kipimo cha Richter lilitokea kwenye pwani ya mashariki ya Taiwan.

Muhtasari

•Chanzo cha tetemeko hilo kinapatikana takriban 18km (maili 11) kusini mwa mji wa Hualien wa Taiwan, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.

•Picha kwenye vyombo vya habari vya ndani zinaonyesha majengo ya makazi yaliyoporomoka na watu wakihamishwa kutoka kwa nyumba na shule zao.

Jengo lililoporomoka kwa kiasi katika mji wa Hualien
Image: BBC

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 katika kipimo cha Richter lilitokea kwenye pwani ya mashariki ya Taiwan siku ya Jumatano, na kutoa tahadhari ya tsunami katika kisiwa hicho na nchi jirani.

Chanzo cha tetemeko hilo kinapatikana takriban 18km (maili 11) kusini mwa mji wa Hualien wa Taiwan, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.

Majengo mengi yameporomoka kwa kiasi huko Hualien na yanaonyeshwa yakiwa yameegemea upnde mmojaNi tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi nchini Taiwan katika miaka 25, wamesema maafisa wa seismolojia.

Kampuni kubwa ya kutengeneza chipsi ya Taiwani TSMC ilisema imehamisha baadhi ya viwanda vyake huko Hsinchu na kusini mwa Taiwan kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wake, lakini ikaongeza kuwa mifumo yake ya usalama inafanya kazi kama kawaida.

TSMC ni mzalishaji mkuu wa semiconductors kwa makampuni makubwa ya ya teknolojia ikiwa ni pamoja na Apple na Nvidia.Katika mji mkuu wa Taipei, video zinaonyesha majengo yakitikiswa kwa nguvu, na kusababisha vitu kutuma kiruka na kutapakaa kila mahali.

Katika maeneo ya ndani ya milima ya Taiwan, video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha tetemeko hilo limesababisha maporomoko makubwa ya ardhi. Kiwango cha uharibifu huo bado hakijajulikana.

Picha kwenye vyombo vya habari vya ndani zinaonyesha majengo ya makazi yaliyoporomoka na watu wakihamishwa kutoka kwa nyumba na shule zao.

Athari za tetemeko hilo pia zimevunja magari na kurusha vitu ndani ya maduka, kulingana na video zilizopeperushwa na kituo cha utangazaji cha TVBS.

Kukatika kwa umeme na kukatika kwa mtandao kumeripotiwa kote kisiwani, kulingana na kikundi cha ufuatiliaji wa mtandao wa NetBlocks.

Tetemeko la ardhi la Jumatano lilipiga saa 07:58 saa za ndani (23:58 GMT) katika kina cha 15.5km na limesababisha angalau mitetemeko tisa yenye ukubwa wa 4 au zaidi.