logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wazazi wa kijana, 15, aliyeua wanafunzi wenza shuleni kwa risasi wafungwa hadi miaka 15 jela

Kijana huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 17 alitekeleza mauaji hayo kwa bunduki akiwa na miaka 15.

image
na Davis Ojiambo

Habari10 April 2024 - 08:25

Muhtasari


  • • Kwa mujibu wa NBC News, Jennifer, 46, na James Crumbley, 47, wakaazi wa jimbo la Michigan nchini Marekani wameuwa kizuizini kwa miaka 2 sasa.
Wanafamilia 4 wametiwa mbaroni kufuatia kifo cha mwanamitindo.

Wazazi wa mvulana wa miaka 15 aliyefyatua risasi kwa wanafunzi wenzake shuleni mnamo 2021 na kuua 4 kati ya 11 waliojeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa NBC News, Jennifer, 46, na James Crumbley, 47, wakaazi wa jimbo la Michigan nchini Marekani wameuwa kizuizini kwa miaka 2 sasa na kesi yao imetamatika mapema wiki hii kwa kujizolea vifungo vya kati ya miaka 10-15 jela.

Wawili hao walipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia kwa kushindwa kumzuia mtoto wao wa kiume, ambaye sasa ana miaka 17, kuwaua wanafunzi wenzake wanne katika tukio baya zaidi la kupigwa risasi shuleni, kila mmoja alihukumiwa siku ya Jumanne kifungo cha miaka 10 hadi 15 jela.

Kesi zao tofauti za mahakama zilimalizika kwa hukumu za hatia Februari na Machi, na kuwafanya wazazi wa kwanza nchini humo kuhukumiwa kutokana na vifo vilivyosababishwa na mtoto wao katika kupigwa risasi kwa wingi.

Mnamo Novemba 30, 2021, vyombo vya habari nchini USA viliripoti kwamba Mtu mwenye bunduki alifyatua risasi katika Shule ya Upili ya Oxford katika Kaunti ya Oakland, Michigan, na kuwafyatulia risasi watu 11. Wanafunzi wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya. Ethan Crumbley, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 kipindi hicho, alikamatwa baadaye kuhusiana na ufyatuaji risasi huo.

Bw. Crumbley pia aliomba msamaha. "Siwezi kueleza ni kiasi gani ningetamani ningejua kinachoendelea kwake au kitakachotokea, kwa sababu ningefanya mambo mengi tofauti," alisema.

Jamaa za baadhi ya wahasiriwa pia walizungumza wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, wakielezea athari kubwa za risasi hiyo katika maisha yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved