logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kimbunga Hidaya: Wawili wafariki, 80 waokolewa katika mafuriko Tanzania

Joseph Mwasabije amesema, "tumewaokoa watu 80 na wawili wamefariki dunia, ambao wote ni wakazi wa Kilwa mkoani Lindi."

image
na Radio Jambo

Burudani06 May 2024 - 03:50

Muhtasari


•Joseph Mwasabije amesema, "tumewaokoa watu 80 na wawili wamefariki dunia, ambao wote ni wakazi wa Kilwa mkoani Lindi."

Watu wawili wamefariki dunia na zaidi ya 80 wameokolewa wilayani Kilwa mkoani Lindi baada ya mvua kubwa kunyesha jana Mei 4, 2024 na kusababisha mafuriko.

Kulingana na Mwananchi Digital, Mafuriko hayo mbali na kusababisha vifo, pia yamesomba madaraja na kukata mawasiliano katika eneo la Somanga.

Akizungumza leo Jumapili, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji, Mrakibu Msaidizi Joseph Mwasabije amesema, "tumewaokoa watu 80 na wawili wamefariki dunia, ambao wote ni wakazi wa Kilwa mkoani Lindi."

Mwasabije amesema waliofariki dunia ni mwanaume na mwanamke ambao bado umri wao haujajulikana.

Wakati huohuo Mwananchi Digital imesema kwamba daraja moja limesombwa na maji na kusababisha mawasiliano kukatika kati ya mikoa ya kusini na Pwani.

Hali hiyo imetokana na madhara ya kimbunga Hidaya kilichosababisha mvua kubwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara na Kisiwa cha Mafia mkoani Pwani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved