logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama akiri kukatisha maisha ya mwanawe mwenye saratani

Kusaidia mtu kufariki dunia, au kumsaidia mtu mwingine kimakusudi kumaliza maisha yake ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

image
na SAMUEL MAINA

Habari04 July 2024 - 12:45

Muhtasari


  • •Antonia Cooper alisema mwanawe alikuwa na saratani ya hatua ya nne na alikuwa katika "maumivu makali" kabla ya kufariki mwaka 1981.
  • •Kusaidia mtu kufariki dunia, au kumsaidia mtu mwingine kimakusudi kumaliza maisha yake ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

Mama mmoja amekiri kwamba alimpa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka saba, ambaye alikuwa akiugua saratani, kipimo kikubwa cha "morphine" ili kukomesha mateso anayopitia na "kumaliza maisha yake kimya kimya."

Antonia Cooper, kutoka Abingdon, Oxfordshire, alisema mwanawe Hamish alikuwa na saratani ya hatua ya nne na alikuwa katika "maumivu makali" kabla ya kufariki mwaka 1981.

Mama huyo sasa anaugua saratani, kulingana na kile alichosema wakati wa mahojiano na BBC Radio huko Oxford, kama sehemu ya jaribio linalolenga kubadilisha sheria na kuruhusu "kusaidiwa kufariki dunia" kwa watu wanaoteseka.

Kusaidia mtu kufariki dunia, au kumsaidia mtu mwingine kimakusudi kumaliza maisha yake, ambayo pia huitwa "euthanasia" au "kumaliza maisha ya mtu kimakusudi", ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

Hali ya mtoto huyo iligunduliwa akiwa na umri wa miaka mitano, na awali madaktari walimwekea makataa ya miezi mitatu, lakini mama yake alisema kwamba baada ya miezi 16 ya matibabu ya saratani "ya kutisha" katika Hospitali ya Great Ormond Street, Hamish aliendelea kuishi lakini alianza kuteseka kwa maumivu makali.

Akaongeza: "Usiku mmoja aliposema ana maumivu makali, nilimwambia: Je! unataka nikuondolee maumivu haya? Akasema: Ndiyo, tafadhali, mama."

Anasema: "Nilimpa, kupitia Hickman catheter, dozi kubwa ya morphine, ambayo ilimaliza maisha yake kwa amani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved