Msako waendelea kuwatafuta wanasoka wa Morocco waliopotea baharini

Wanasoka wawili waliotoweka katika pwani ya kaskazini mwa nchi hiyo ya Mediterania siku ya Jumamosi.

Muhtasari

•Huduma za dharura ziliwaokoa watu watatu baada ya kisa hicho, lakini wachezaji wakuu Abdellatif Akhrif, 24, na Salman El-Harrak, 18, hawajapatikana.

Image: HISANI

Klabu ya Morocco Ittihad Tanger imeiambia BBC kuwa msako unaendelea kuwatafuta wanasoka wawili waliotoweka katika pwani ya kaskazini mwa nchi hiyo ya Mediterania siku ya Jumamosi.

Wahudumu watano wa Ligi Kuu ya Morocco wanashiriki katika msako wa meli ya kifahari iliyokodishwa katika eneo la mapumziko la ufuo la M'diq - kaskazini mwa jiji la Tetouan, waliyokuwa wakisafiria.

Huduma za dharura ziliwaokoa watu watatu baada ya kisa hicho, lakini wachezaji wakuu Abdellatif Akhrif, 24, na Salman El-Harrak, 18, hawajapatikana.

Oussama Aflah, Soumaimane Dahdouh na Abdelhamid Maali, mchezaji wa kimataifa wa Morocco wa kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 20, waliokolewa baada ya kuwa baharini kwa saa kadhaa.

Aflah namesajiriwa na klabu, wakati Dahdouh na Maali walikuwa wanakichukuliwa kuwa ni wachezaji wazuri wa timu wa akiba.

Rais wa Ittihad Tanger, Mohamed Cherkaoui alithibitisha kuwa "utafutaji wa wachezaji waliopotea bado unaendelea".

Pia amewataka mabaharia na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii kuendelea kuwa makini na taarifa wanazotoa kuhusu wawili hao.