Binti ya rais atumai kujitokeza kwake kutabadilisha sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 27 alisambaza picha yake akimbusu mwanamke mwingine wiki iliyopita, jambo lililozua hisia tofauti nchini Cameroon.

Muhtasari
  • Brenda Biya aliliambia gazeti la Le Parisien kwamba kulikuwa na watu wengi katika hali kama yake na anatumai kuwatia moyo.

Binti wa rais wa Cameroon amesema anatumai kuwa kujitokeza kwake kama anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja kunaweza kusaidia kubadilisha sheria inayopiga marufuku mahusiano ya jinsia moja nchini mwake.

Brenda Biya aliliambia gazeti la Le Parisien kwamba kulikuwa na watu wengi katika hali kama yake na anatumai kuwatia moyo.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 27 alisambaza picha yake akimbusu mwanamke mwingine wiki iliyopita, jambo lililozua hisia tofauti nchini Cameroon.

"Nina kupenda kupita maelezo na ninataka ulimwengu ujue," alisema kwenye ujumbe wa Instagram na picha yake wakikumbatiana na mwanamitindo wa Brazil Layyons Valença.

Katika mahojiano na gazeti la Ufaransa Le Parisien, alisema hakuwa amemjulisha mtu yeyote katika familia yake kabla ya kuweka ujumbe huo mtandaoni.

"Kutoka nje ni fursa ya kutuma ujumbe mzito," alisema.

Aliongeza kuwa anaona sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja, ambayo ilikuwepo kabla ya babake kuingia madarakani, kwamba "si ya haki na ninatumai kwamba simulizi yangu itaibadilisha hilo".

Paul Biya, 91, amekuwa rais wa Cameroon tangu 1982 na ni mmoja wa viongozi waliokaa madarakani muda mrefu zaidi barani Afrika.

Biya alisema amekuwa na mwanamitindo huyo wa Brazil kwa muda wa miezi minane na tayari amempeleka Cameroon mara tatu bila kuwaambia familia yake walikuwa kwenye uhusiano.