Burkina Faso imekuwa nchi ya hivi punde zaidi barani Afrika kuharamisha mapenzi ya jinsi moja.
Wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri, serikali inayoongozwa na jeshi iliidhinisha sheria inayopiga marufuku ndoa za mapenzi ya jinsi moja na mila kama hiyo.
Waziri wa sheria wa Burkina Faso Edasso Rodrigue Bayala amesema sheria hiyo mpya inatambua ndoa za kimila na kidini pekee chini ya sajili yake ya kiraia.
Sheria hiyo sasa itaendelea ili kuidhinishwa na bunge kabla ya kutiwa saini na Ibrahim Traore - kiongozi wa mapinduzi ambaye alisimamia mkutano wa baraza la mawaziri.
Taifa hilo la Afrika Magharibi lilikuwa miongoni mwa nchi ishirini na mbili kati ya hamsini na nne zilizoruhusu mapenzi ya jinsi moja ambayo yanaadhibiwa kwa kifo au kifungo cha muda mrefu jela kwa nchi nyingine.
Uganda ilipitisha mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya LGBTQ mwezi Mei mwaka jana.