•Biden alitangaza kuwa hata ingawa anahisi nafuu, atakuwa akijitenga kwa muda huku akipokea matibabu ili kupata nafuu kabisa.
•"Nitakuwa nikijitenga ninapopona, na wakati huu nitaendelea kufanya kazi ili kufanya kazi kwa watu wa Amerika."
Rais wa Marekani Joe Biden amefichua kuwa hayuko vizuri kiafya.
Katika taarifa ambayo alitoa usiku wa kuamkia Alhamisi, rais huyo wa 46 wa Marekani alifichua kwamba alipatikana na COVID-19 mnamo Jumatano alasiri.
Biden alitangaza kuwa hata ingawa anahisi nafuu, atakuwa akijitenga kwa muda huku akipokea matibabu ili kupata nafuu kabisa.
"Nilipimwa na kupatikana na COVID-19 mchana huu, lakini ninahisi vizuri na ninashukuru kila mtu kwa kunitakia heri," Biden alisema kupitia mtandao wa Twitter.
Aliongeza, "Nitakuwa nikijitenga ninapopona, na wakati huu nitaendelea kufanya kazi ili kufanya kazi kwa watu wa Amerika."
Haya yanajiri siku chache tu baada ya mpinzani wake mkuu katika uchaguzi mkuu ujao wa Marekani, Donald Trump, kunusurika katika jaribio la mauaji.
Siku ya Jumamosi, Julai 13, Donald Trump alinusurika jaribio la mauaji wakati wa mkutano wa kisiasa katika mji wa Butler, Pennsylvania.
Rais huyo wa zamani wa Marekani, ambaye anawania muhula wa pili, alisema ni jambo lisilo la kuaminika kwamba jambo kama hilo linaweza kutokea nchini Marekani.
Alisema risasi ilipenyeza kwenye sehemu ya juu ya sikio lake la kulia katika tukio hilo la kupigwa risasi.
“Nilipigwa risasi na risasi iliyopenya sehemu ya juu ya sikio langu la kulia... Kuvuja damu nyingi kulitokea, kwa hiyo nikagundua kilichokuwa kikiendelea. Mungu Ibariki Marekani!” alisema.
Mshambuliaji wa kiume alipigwa risasi na kuuawa na mjumbe wa Huduma ya Siri baada ya jaribio la kumuua Trump katika hafla hiyo.
Mshambuliaji huyo alimuua mtazamaji mmoja katika mkutano huo, na wengine wawili walijeruhiwa vibaya, kulingana na Huduma ya Siri.