Harris anaweza kutumia fedha za kampeni za Biden

Michango ya kampeni ya Biden imefikia $96m mwanzoni mwa Julai, kulingana na nyaraka FEC.

Muhtasari
  • Kampeni sasa inamtaja rasmi Makamu wa Rais Kamala Harris kama mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa 2024, kulingana na barua iliyotumwa kwa Tume ya Uchaguzi wa shirikisho au FEC.

Kampeni za kuchaguliwa tena kwa Rais Joe Biden zimechukua hatua rasmi ya kupitisha jina la "Harris kugombea Urais".

Kampeni sasa inamtaja rasmi Makamu wa Rais Kamala Harris kama mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa 2024, kulingana na barua iliyotumwa kwa Tume ya Uchaguzi wa shirikisho au FEC.

Hii ni hatua kubwa, kwani Biden na Harris wanashiriki kamati ya kampeni.

Sasa anaweza kuendelea kutumia fedha za uchaguzi mkuu ambazo kampeni ya Biden ilikuwa imechangisha hapo awali.

Michango ya kampeni ya Biden imefikia $96m mwanzoni mwa Julai, kulingana na nyaraka FEC.

Chama na kamati kadhaa za utekelezaji wa kisiasa zina pesa za ziada ambazo Harris anapania kupata kwa kuwa mteule rasmi wa chama.

Trevor Potter, mwenyekiti wa zamani wa FEC ambaye anaongoza Kituo cha Kisheria cha Kampeni, alisema "mteule anayetarajiwa kujiuzulu miezi kadhaa kabla ya Siku ya Uchaguzi sio tukio la kawaida, lakini pia sio tatizo".

Harris anaweza kutumia fedha za kampeni za Biden kwa sababu walishiriki kamati ya kampeni, lakini "sheria ni tofauti" kwa tikiti ambayo haijumuishi makamu wa rais, Potter alisema.