•Mbwa takriban 400 wanahofiwa kufa mwezi mmoja uliopita baada ya kula mahindi yenye sumu na huenda binadamu wakawa hatarini pia.
Mbwa takriban 400 wanahofiwa kufa mwezi mmoja uliopita nchini Zambia baada ya kula mahindi yenye sumu na huenda binadamu wakawa hatarini pia, waziri wa afya wa nchi hiyo amesema.
Elijah Muchima alitangaza kwamba takriban nusu ya sampuli 25 zilizochukuliwa kutoka kwa kampuni za kusaga mahindi zilipatikana kuwa na viwango vya juu sana vya aflatoxin, dutu yenye sumu inayozalishwa na kuvu.
Mahindi ni chakula kikuu nchini Zambia na Bw Muchimi alisema matokeo ya sampuli zilizochukuliwa "yanatia wasiwasi mkubwa kutokana na athari nyingi za kiafya kwa [watu]".
Shirika la Chakula Duniani (WHO) limesema kuwa kuna ushahidi kwamba sumu kuvu inaweza kusababisha saratani ya ini kwa binadamu.