Mwanasiasa Bobi Wine apigwa risasi mguuni

Bw Ssenyonjo aliambia BBC kwamba Bobi Wine alipigwa risasi na 'polisi aliyevalia sare'.

Muhtasari

•Robert Kyagulanyi, maarufu kama "Bobi Wine," amepigwa risasi mguuni, kwa mujibu wa msaidizi wake binafsi, Najja Ssenyonjo.

Bobi Wine
Image: MAKTABA

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu kama "Bobi Wine," amepigwa risasi mguuni, kwa mujibu wa msaidizi wake binafsi, Najja Ssenyonjo.

Bw Ssenyonjo aliambia BBC kwamba Bobi Wine alipigwa risasi na 'polisi aliyevalia sare' na kwa sasa anapokea matibabu katika hospitali ya Nsambya katika mji mkuu, Kampala.

Alisema tukio hilo lilitokea wakati Bobi Wine alikuwa akikutana na mawakili wake.

Taarifa kwenye akaunti ya X ya Bobi Wine ilisema, "@HEBobiwine amepigwa risasi mguuni na polisi huko Bulindo."

Maelezo bado yanatolewa, na hadi kufikia sasa hakuna taarifa rasmi ambayo imetolewa na polisi au chama cha upinzani.