Chombo cha anga za juu Boeing Starliner charudi Duniani, bila wanaanga

Chombo tupu kilisafiri kwa hali ya uhuru baada ya kujiondoa kutoka kwenye obit (uzio)yake.

Muhtasari

•Wanaanga ambao chombo hicho kilipaswa kuwabeba wamesalia nyuma kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

Image: BBC

Chombo cha anga za juu cha Boeing's Starliner kimekamilisha safari yake ya kurejea Duniani - lakini wanaanga kilichopaswa kuwabeba wamesalia nyuma kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

Chombo tupu kilisafiri kwa hali ya uhuru baada ya kujiondoa kutoka kwenye obit (uzio)yake.

Chombo hicho ambacho kilikumbwa na matatizo ya kiufundi baada ya kufyatuliwa kuelekea anga za mbali kikiwa na wanaanga Butch Wilmore wa Nasa na Suni Williams, kilionekana kuwa ni hatari sana kuwarudisha wanaanga hao nyumbani.

Badala yake watarudi katika katika chombo cha SpaceX Crew Dragon, mwezi Februari, na hivyo kuongeza muda wao wa kukaa katika anga za mbali kutoka siku nane zilizotarajiwa hadi miezi minne.

Baada ya Starliner kurejea, msemaji wa Nasa alisema alifurahishwa na kutua kwa mafanikio kwa chombo hicho, lakini alitamani lsafari ingeenda kama ilivyopangwa awali.

Safari ya kurudi ilichukua saa sita. Baada ya kuingia tena kwenye angahewa ya Dunia na miavuli ya miamvuli ilitumiwa kupunguza kasi yake ya kutua katika kituo cha White Sands Space Harborhuko New Mexico siku ya Jumamosi saa tano na dakika moja za usiku kwa saa za eneo.