48 waangamia kufuatia mlipuko wa lori la petroli

Watu takriban 48 waripotiwa kupoteza maisha yao, kufuatia mlipuko wa gari la petroli nchni Nigeria

Muhtasari

•Watu 48 wakisiwa kuaga dunia baada ya gari la petroli kugongana na lori liliokuwa limebeba wauza mifugo,Nigeria.

•Miili ilichomeka kwa kiasi cha kutotambulika vile vile ng'ombe 50 kuaga katika kisa hicho.

Tanker explode
Image: Hisani

Watu takriban 48 wameripotiwa kupoteza maisha yao baada ya gari la petroli kuilipuka nchni Nigeria.

Hii ilitokana na gari hilo kugongana na lori katika barabara ya Lapai-Agaie, Mnamo Jumapili 8, Septemba 2024.

Kulingana na shirika la kudhibiti matukio ya dharura la Nigeria,inasemekana gari ilo lilogongana ana kwa ana na lori ambalo linasemekana lilikuwa limewabeba wauza mifugo.

Kutokana na shahidi ambaye alishuhudia ajali hiyo, ni kwamba mgongano huo ulisababisha moto mkubwa ulifuatiwa na mlipuko.

Aidha,kutokana na mlipuko huo ulisababisha moto kusambaa na kuteketeza mali ya dhamana kubwa na kuacha eneo la tukio mahame.

Gavana wa jimbo la Niger Mohammed Umar Bago, ametoa rambi rambi zake kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Taarifa zinaashiria kuwa kwenye ajali hiyo,miili ilichomeka kupita kiwango cha kutambulika  vile vile ng'ombe 50 kuteketea.

Ni tukio ambalo limelemaza shughuli ya kutambua miili ya marehemu, na kusababisha fedheha kwa familia za waliopoteza maisha

Kutokana na ajali hiyo sasa ,familia zilizopoteza wapendwa wao sasa zimefikwa na majonzi, huku taifa lote kwa ujumla likizidi kuomboleza.

Wazima moto walifika eneo la tukio ila kwa kuchelewa na kuzima mabaki ya moto hili kuzuia kusambaa zaidi.