Mwanamume amchoma mtoto kwa kahawa moto

Mshukiwa mkuu alitorokea nchini Sydney kupitia uwanja wa ndege siku sita baada ya kufanya kitendo hicho.

Muhtasari

• Mtoto wa miezi tisa alichomwa kwa kahawa moto akiwa katika sehemu ya kutulia pamoja na wazazi wake.

• Mshukiwa alitoroka kwa kuabiri ndege siku sita baadaye na polisi wa Queensland wanashirikiana na polisi wa kimataifa kumsaka mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 33.

Maji moto
Maji moto
Image: BBC

Polisi wa Australia wanashirikiana na polisi wa kimataifa kumsaka mwanamume anayedaiwa kumwagia mtoto mchanga kahawa moto jijini Brisbane mwezi uliopita.

Kulingana na polisi ambao tayari wametoa kibali cha kukamatwa kwa mwanamume huyo, wamesema kuwa jamaa huyo aliyeonekana kwa kamera za CCTV alimwagia mtoto wa miezi tisa kahawa hiyo iliyokuwa inachemka na kumwacha na majeraha mabaya usoni na miguuni.

Taarifa zaidi za polisi wa Queensland zilizotelewa Jumatatu zimeeleza kuwa mshukiwa mkuu alitorokea nchini Sydney kupitia uwanja wa ndege siku sita baada ya kufanya kitendo hicho ikiwa saa kumi na mbili kabla ya polisi kuhakiki utambulisho wake.

Ijapokuwa lengo la mwanamume huyo kumwagia mtoto kahawa moto halijajulikana, polisi wamesema mwanamume huyo atashtakiwa kwa kosa la kukusudia kusababisha madhara makubwa ya mwili, kosa ambalo linaweza kumweka gerezani kwa kifungo cha maisha.

Aidha katika ujumbe kwa vyombo vya habari leo Jumatatu, wazazi wa mtoto wamekiri kuwa hali yake iko shwari japo anahitaji matibabu zaidi wa kurekebisha ngozi.