Watatu wafariki baada ya shambulizi Ukraine mashariki

Wafanyakazi watatu wa shirika la msalaba mwekundu waaga dunia baada ya lori lao kushambuliwa na kikosi cha kijeshi cha Russia.

Muhtasari

•Watu watatu ambao ni wafanyakazi wa shirika la kimaifa la msalaba mwekundu wapoteza maisha yao baada ya lori lao kulipuliwa na jeshi ya Russia.

•Katika tukio hilo,watu wengine wawili walipata majeraha kutokana mlipuko wa lori hilo,huku viongozi wa eneo la Viroliubivka wakisema wakaazi eneo hilo wako kwenye hatari.

ICR TRUCK BURNING
Image: HISANI

Watu watatu  wa shirika la msalaba mwekundu wamethibitishwa kufariki baada ya lori lao kushambuliwa na kikosi cha kijeshi cha Russia kushambulia lori hilo ambalo ni la kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu.

Kisa hicho kilitokea tarehe 12 septemba 2024, ambacho kilitekelezwa na jeshi la taifa hilo la Russia na kusababisha lori hilo kulipuka na kupelekea watatu hao kupoteza maisha yao.

Kufuatia taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa rais wa taifa hilo ,tukio hilo lilitokea katika kijijin cha Viroliubivka karibu na eneo la Donetsk.

Kutokana kwa kupigwa bomu kwa gari hilo,watatu walifariki hjapo kwa hapo na kusababisha majeraha kwa wafanyakazi wengine wawili kweye shambulizi hilo.Ni taarifa ambayo ilithibitishwa na mojawapo ya viongozi kutoka taifa hilo la Ukraine.

Tukio hilo  linashtumiwa kuwa limechangiwa sana na mgogoro uliopo baina ya mataifa hayo ,ni jambo ambalo rais wa taifa hilo la Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametilia mkazo kupitia mtandao weake wa X.

Kufuatia shambulizi hilo,limewatia wakaazi wa eneo la Viroliubivka na woga hasa kutokana na mabomu ambayo yalikuwa yanarushwa na jeshi ya Russia.Kiongozi wa eneo hilo  Vadym Filashkin ameongeza kupitia mtandao wa Telegram huku baadhi ya watu kutoka eneo hilo wakiuguza majeraha.