Zaidi ya 100 wafariki kufuatia mafuriko hatari nchini Myanmar

Mafuriko yaliyoanza wiki jana yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundo misingi na vifo vya watu zaidi ya mia moja

Muhtasari

• Kimbunga cha Typhoon Yagi kinahofiwa kusambaa hata zaidi  katika siku za usoni hadi magharibi mwa Pasifiki.

Image: HISANI

Zaidi wa watu mia moja wamefariki kutokana na mafuriko ya baada ya mvua mkubwa maarufu kama Typhoon Yagi kunyesha nchini Myanmar.

Hili limedhibitishwa na jeshi la Myanmar.

Taarifa hiyo ya jeshi imesema kuwa watu laki tatu na elfu ishirini wamekosa makao huku idadi ya watu 64 bado hawajulikani walipo kufikia wakati wa kuchapisha taarifa hii.

Kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari ya taifa la Myanmar, mafuriko hayo yalianza Jumatatu Septemba 9 na kufikia Ijumaa Septemba 13, tayari watu zaidi ya sabini walikuwa wameripotiwa kuaga dunia.

Ofisi ya umoja wa mataifa ya utaratibu wa masuala ya kibinadamu imetaarifu kuwa jiji kuu la Myanmar Naypyidaw ndio imeathirika zaidi.

Sehemu nyingine pia ziliathirika ikiwemo Magway, Bago, Mandalay, Kayah, Kayin, Mon na Shan. 

Tayari wizara ya mawasiliano ya Myanmar imetangaza kupeleka wafanyakazi wa afya katika maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko pamoja na chakula cha msaada kwa waathiriwa.

Hta hivyo shughuli za kukusanya data na kufikia sehemu nyingine zilizoathirika zinakumbwa na matatizo kwani miundo misingi muhimu kama vile barabara za kufika maeneo hayo zimeharibika.

Wanasayansi wanaonya kuwa kimbunga icho cha Typhoon Yagi huenda kitasambaa hata zaidi hadi maeneo ya  magharibi ya Pasifiki katika siku za usoni.