Mahakama ya Urusi imetoza Google faini ya rubles 200 - mbili ikifuatiwa na sufuri 36 - kwa kuzuia njia za vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kwenye YouTube.
Kwa maneno ya dola hiyo ina maana kwamba Google imeambiwa ilipe $20,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000… kiwango ambacho kinazidi GDP ya dunia mzima.
Licha ya kuwa moja ya kampuni tajiri zaidi duniani, hiyo ni zaidi ya dola trilioni 2 za Google.
Kwa kweli, ni kubwa zaidi kuliko jumla ya Pato la Taifa la dunia, ambalo linakadiriwa na Shirika la Fedha la Kimataifa kuwa $110 trilioni, BBC walibaini.
Faini hiyo imefikia kiwango cha juu sana kwa sababu - kama shirika la habari la serikali Tass lilivyoangazia - inaongezeka kwa kasi kila wakati.
Kulingana na Tass, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikiri "hawezi hata kutamka nambari hii" lakini akahimiza "wasimamizi wa Google kuzingatia."
Chombo cha habari cha Urusi RBC kinaripoti faini hiyo kwenye Google inahusiana na kizuizi cha maudhui ya vituo 17 vya habari vya Kirusi kwenye YouTube.
Wakati hii ilianza mnamo 2020, iliongezeka baada ya uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine miaka miwili baadaye.
Hiyo ilishuhudia kampuni nyingi za Magharibi zikijiondoa Urusi, na kufanya biashara huko pia kumezuiliwa sana na vikwazo.
Vyombo vya habari vya Urusi pia vilipigwa marufuku barani Ulaya - na kusababisha hatua za kulipiza kisasi kutoka Moscow.
Kwa hakika hakuna uhuru wa vyombo vya habari nchini Urusi, huku vyombo huru vya habari na uhuru wa kujieleza vikiwa vimepunguzwa sana.