Makamu wa rais wa Equitorial Guinea Teodoro Obiang Nguema amesema kuwa serikali ya nchi hiyo itawafuta kazi maafisa na watumishi wote wa umma wa taifa hilo ambao ni miongoni mwa wanawake waliorekodiwa katika sakata ya ngono na Mkurugenzi mkuu wa shirikala kitaifa la upelelezi wa fedha (ANIF) la nchini Equitorial Guinea.
Zaidi ya wanawake
400 wanaripotiwa kushiriki mapenzi na mkurugenzi huyo mkuu katika sehemu
tofauti tofauti ikiwemo afisi za serikali na nyumbani kwa mshukiwa ambaye
alikamatwa na polisi na anasubiria kufunguliwa mashtaka.
Katika video
ambazo zimesambaa mitandaoni, Mkurugenzi huyo kwa jina Baltasar Ebang Engonga
mwenye umri wa miaka 54, amekuwa akishiriki mapenzi na wanawake wengi ikiwemo
wake wa maafisa wakuu katika serikali ya Equitorial Guinea.
Katika kanda za
video alizokuwa akirekodi, Engonga alionekana akifanya mapenzi na wake wakiwemo
mke wa mkuu wa ulinzi wa rais wa nchi hiyo, mtoto wa mkuu wa jeshi la polisi,
mke wa mwanasheria mkuu, binamu yake, mke wa mlinzi wake, mke wa mjomba wake
ambaye ni mjamzito kati ya wake wa watu wengine mashuhuri nchini humo.
Kupitia ukurasa
wa X, makamu wa rais wa nchi hiyo amesema kuwa serikali tayari imeanza
kuwachukulia hatua maafisa ambao wameshiriki mapenzi katika ofisi za wizara
mbali mbali kwa kuwaachisha kazi mara moja.
Makamu wa rais
Nguema amesema kuwa serikali itawachukulia hatua kali dhidi ya visa hivyo,
akiongeza kuwa ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za maadili na sheria ya maadili ya
umma.
āMaadili na heshima ni mambo ya msingi katika utawala wetu
na hatutaruhusu tabia ya kutowajibika ihatarishe imani ya umma.ā Alisema makamu huyo wa rais.
Aidha
katika juhudi za kukabiliana na visa kama hivyo, makamu huyo wa rais amesema
kuwa serikali itawekeza katika kuweka kamera za CCtv katika kila ofisi
inayoomilikiwa na taasisi za serikali.
Makamu
rais Teddy Nguema serikali imelazimika kuchukua hatua hiyo kuhakikisha kwamba
sheria kwa maafisa wa umma inafuatwa ili kuondoa tabia hiyo mbovu.
Teodoro Obiang vile
vile amesema kamwe serikali haitakubali kosa lolote linalodhalilisha uadilifu wa
utawala wa Equitorial Guinea na wale wanaojihusisha na vitendo hivi
watakabiliwa na hatua kali.