Shirikala
mpango wa chakula duniani WFP limearifu kuwa takribani watu bilioni tatu kote
duniani huenda kufikia mwaka wa 2030, wataishi katika maeneo ambayo yana hatari
kubwa ya kushuhudia mabadiliko ya hali ya hewa.
Kulingana
na shirika hilo, mabadiliko ya hali ya hewa inapelekea mamilioni ya watu
duniani kukumbwa na njaa kila mwaka kutokana na kuongezeka kwa mabadiliko ya hali
ya hewa inayosambaratisha hali ya kibinadamu ambayo tayari iko mashakani.
WFP
imesema kwamba katika maeneo ambayo yapo katika hatari kubwa ya kushuhudia mabadiliko
ya hali ya hewa, takribani watu bilioni tatu watakumbwa na janga hilo kufikia
mwaka wa 2030.
Shirika
hilo limeongeza kusema kwamba matukio makali ya hali ya hewa yanayoshuhidiwa
katika baadhi ya nchi duniani, inaathiri watu mara tatu zaidi ikilinganishwa na
sehemu nyingine kila mwaka. WFP aidha imesikitikia kuwa mataifa ambayo yapo
katika hatari zaidi yanakosa kupata ufadhili wa kupambana na mabadiliko hayo
kwa kiwango cha chini zaidi cha mara 80 kulinganishwa na mataifa mengine.
Hata
hivyo shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limeshauri kwamba ili kupigana
na njaa, ni lazima juhudi za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa
yatekelezwe kwa haraka katika sehemu zilizo kwenye shinikizo kubwa.