logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Takriban watu 34 wameuawa katika shambulizi la Israel kaskazini mwa Gaza

Wengi wa waliofariki ni wanawake na watoto, huku makumi ya watu wakihofiwa kuwa chini ya vifusi.

image
na BBC NEWS

Kimataifa18 November 2024 - 09:24

Muhtasari


  • Jeshi la Israel limesema limekuwa likishambulia maeneo ya wanamgambo kaskazini mwa Gaza, ikiwemo Beit Lahia.

Mashambulizi ya anga ya Israel kwenye jengo la ghorofa tano la makazi huko Beit Lahia kaskazini mwa Gaza yamesababisha vifo vya takriban watu 34, shirika la ulinzi wa raia la eneo hilo linasema.

Shirika hilo, lililonukuliwa na AFP, lilisema wengi wa waliofariki ni wanawake na watoto, huku makumi ya watu wakihofiwa kuwa chini ya vifusi. Watu saba pia walijeruhiwa.



Mashambulizi ya anga ya Israel kwenye jengo la ghorofa tano la makazi huko Beit Lahia kaskazini mwa Gaza yamesababisha vifo vya takriban watu 34, shirika la ulinzi wa raia la eneo hilo linasema.

Shirika hilo, lililonukuliwa na AFP, lilisema wengi wa waliofariki ni wanawake na watoto, huku makumi ya watu wakihofiwa kuwa chini ya vifusi. Watu saba pia walijeruhiwa

Jeshi la Israel limesema limekuwa likishambulia maeneo ya wanamgambo kaskazini mwa Gaza, ikiwemo Beit Lahia, katika jaribio la kuwazuia Hamas kujipanga upya.

Kwingineko, katikati mwa Gaza mashambulizi matatu tofauti dhidi ya kambi za wakimbizi yamesababisha vifo vya watu 15, huku wengine watano wakiuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Israel huko Rafah kusini, ulinzi wa raia uliongeza.

"Uwezekano wa kuokoa waliojeruhiwa unapungua kwa sababu ya ufyatuaji risasi unaoendelea na mizinga," msemaji wa ulinzi wa raia Mahmud Bassal alisema.

Kilichosalia kwenye jengo la makazi huko Beit Lahia ni rundo la vifusi, na saruji iliyovunjika na vipande vya chuma vilivyosokotwa vinavyotoka kwenye magofu.

Mwanamume mmoja, ambaye familia yake iliishi katika jengo hilo, lakini alikuwa anakaa mahali pengine, alisema, akinukuliwa na AFP: "Sote tulifikiri kwamba kifo kilikuwa karibu."

"Eneo lote lilikuwa linatetemeka."

Jeshi la Israel lilisema mashambulizi yake kaskazini mwa Gaza - yaliyoanzia Jabalia na kuzidishwa hadi Beit Lahia - yalihusisha mashambulizi kadhaa usiku kucha kwa kile ilichokiita "lengo la kigaidi katika eneo hilo".

Iliongeza katika taarifa kwamba "kumekuwa na juhudi za kuendelea kuwaondoa raia kutoka eneo la vita ".

Lakini wakazi wengi wa eneo hilo hawataki kuacha nyumba zao. Bw Bassel alisema familia sita ziliishi katika jengo lililoharibiwa huko Beit Lahia.

Mwanamke mmoja katika eneo hilo alielezea hasira yake kwa BBC News.

"Tumewakosea nini watu, tumewasababishia madhara gani? Tumefanya kosa gani, tunakaa majumbani mwetu, mbona mnatufukuza?"



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved