Umoja wa mataifa (UN) umeripoti kwamba takribani watu 1,062 waliuliwa au kupata majeraha ndani ya mwezi Novemba nchini Ukraine katika vita vinavyoendelea kushuhudiwa baina ya Ukraine na Urusi.
Ripoti hiyoiliyotolewa Disemba 10, imesema kwamba angalau watu 165 waliuliwa huku watu wengine 887 wakipata majeraha katika mwezi huo pekee. Kwenye idadi hiyo, watoto wanane waliangamia na hamsini na saba wakipata majeraha.
Idadi hiyo aidha ni chache ikilinganishwa na maafa yaliyotukia mwezi Oktoba ila ilibainika kwamba idadi hiyo ya Novemba ilikuwa kubwa ikilinganishwa na Novemba ya mwaka 2023. Katika mwaka 2023 mwezi Novemba, idadi ya raia waliopoteza maisha yao ilikuwa 113 huku raia 363 walipata majeraha.
Kwenye ripoti hiyo, Umoja wa mataifa umeripoti kwamba jeshi ya Urusi lilianza tena uvamizi wa kiwango kikubwa dhidi ya Ukraine, likielekeza uvamizi wake uliopangwa kwa miundo misingi ya kawi ya Ukraine shambulizi la karibuni likiwa katika mwezi wa Agosti.
Vile vile, Urusi ilitekeleza mashambulizi mengine 2 ndani ya mwezi Novemba dhidi ya Ukraine ambapo vifaa 24 vya kuzalisha na kusambaza nguvu za umeme vilishambuliwa kwenye maeneo 13. Vifaa hivyo ilikuwemo vifaa vya kubadilisha kawi kutoka mitambo ya nyuklia ambazo kushambuliwa kwake kulisababisha ukosefu wa nguvu za umeme katika sehemu nyingi za nchi hiyo.
Aidha data ya UN imeashiria kwamba asilimia 42 ya waathiriwa ambayo ni vifo 65 na majeruhi 372, ilitokana na utumiaji wa zana za vita za masafa marefu kama vile makombora na silaha za kuzurura zilizofyatuliwa na vikosi vya Urusi.
Ripoti hii inajiri wakati ambapo rais mteule wa Marekani Donald Trump ametofautiana na taifa la Ukraine kutumia makombora yanayotengenezwa nchini Marekani dhidi ya Urusi akisema kwamba utumiaji wa makombora hayo unazidisha kuchacha kwa vita hivyo.
Trump ambaye ataapishwa rasmi mwakani kama rais wa Marekani ameelezea haja ya kusitisha haraka vita hivyo ambavyo vimedumu kwa karibu miaka mitatu.
Mnamo Jumatatu, Msimamizi wa shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa Samantha Power alitia saini dhamana ya kifedha inayounga mkono mkopo wa serikali ya Marekani wa kuongeza mapato ya kiajabu ya Dola bilioni 20 (ERA) kwa Serikali ya Ukraine katika juhudi za sehemu ya dhamira ya G7 ya kuleta ufadhili wa jumla wa dola bilioni 50 chini ya mpango wa mkopo wa ERA kushughulikia mahitaji muhimu na ya haraka ya ufadhili kwa Ukraine katika mapambano yake dhidi ya uvamizi haramu wa Urusi.
Marekani kupitia utawala wa Biden na Harris unalenga kuiweka Ukraine katika nafasi imara zaidi na itaendelea kuchukua hatua za maana katika kuisaidia Ukraine kupigania mustakabali unaostahili.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ya ofisi
ya mahusiano ya vyombo vya habari iliyotolewa Jumanne, Disemba 10, 2024.