logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Shirika la Reli Tanzania kununua injini za dizeli kupiga jeki shughuli za SGR

Hatua hii inalenga kukabiliana na tatizo la kukatika kwa mara kwa mara kwa umeme kunakoyakumba maeneo mengi ya nchi hiyo.

image
na BBC NEWS

Kimataifa14 December 2024 - 08:30

Muhtasari


  • ''Fedha za injini tayari zimetengwa katika bajeti yetu. Mchakao wa ununuzi unaendelea na tunatarajia kupata injini mwaka ujao'', amesema Masanja kadogosa


Shirika la reli nchini Tanzania (TRC) limesema litanunua injini zinazotumia dizeli ili kupiga jeki shughuli za usafiri wa leri nchini humo.

Hatua hii inalenga kukabiliana na tatizo la kukatika kwa mara kwa mara kwa umeme kunakoyakumba maeneo mengi ya nchi hiyo.

''Fedha za injini tayari zimetengwa katika bajeti yetu. Mchakao wa ununuzi unaendelea na tunatarajia kupata injini mwaka ujao'', amesema Masanja kadogosa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini Tanzania.

Hivi karibuni ulifanyika uzinduzi reli ya umeme na jengo kama madini adimu ya tanzanite, jijini Dar es Salaam, kuashiria mwanzo mpya katika sekta hiyo ya safari reli nchini Tanzania.

Treni zinazotumia umeme nchini Tanzania, hubeba abiria kutoka mji wa kibiashara Dar es Salaam hadi mji mkuu, Dodoma, kwa safari ya chini ya saa nne, nusu ya muda ukisafi kwa barabara.

Ujenzi huo wa Reli ya Standard Gauge (SGR) yenye urefu wa kilomita 2,560 (maili 1,590) inayotarajiwa kuunganisha miji muhimu na kuunganisha nchi jirani Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved