logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu wawili wauawa na mwanafunzi wa kike kwa kupigwa risasi katika shule ya Kikristo

Mshambuliaji huyo alikuwa shule ya Abundant Life Christian School kabla ya kufyatua risasi na alikutwa amefariki katika eneo la tukio.

image
na BBC NEWS

Kimataifa17 December 2024 - 12:04

Muhtasari


  • Mamlaka inasema mshambuliaji huyo alikuwa shule ya Abundant Life Christian School kabla ya kufyatua risasi na alikutwa amefariki katika eneo la tukio.


Mwanafunzi mmoja amefyatua risasi katika shule ya kibinafsi ya Kikristo katika jimbo la Wisconsin Marekani, na kujeruhi watu sita na kumuua mwalimu na mwanafunzi kijana.

Mkuu wa Polisi wa Madison Shon Barnes alimtaja mshambuliaji huyo Jumatatu usiku kuwa mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 15 katika shule hiyo.

Mamlaka inasema mshambuliaji huyo alikuwa shule ya Abundant Life Christian School kabla ya kufyatua risasi na alikutwa amefariki katika eneo la tukio.

Wanafunzi sita walijeruhiwa, wakiwemo wawili waliopata majeraha yanayo tishia maisha yao.

Mwanafunzi wa gredi ya pili alikuwa wa kwanza kupiga simu, kulingana na Mkuu wa Polisi Barnes.

"Leo ni siku ya huzuni sio tu kwa Madison, kwa nchi yetu yote," Barnes alisema.

Aliongeza kuwa polisi hawajabaini sababu za tukio hilo la ufyatuaji risasi, na familia ya mshukiwa ilikuwa ikishirikiana na uchunguzi.

Alisema bado haijabainika jinsi mshambuliaji huyo alipata bunduki.

Hata hivyo, matukio ya ufyatuaji risasi kwa wingi na wanawake ni nadra na ufyatuaji risasi shuleni unaofanywa na washambuliaji wa kike ni vigumu sana kutokea.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved