logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi aliyelewa awaachilia washukiwa 13 ili wakasherehekee mwaka mpya

Inspekta wa upelelezi Titus Phiri alikamatwa baada ya kuwaachilia washukiwa hao.

image
na BBC NEWS

Kimataifa03 January 2025 - 08:31

Muhtasari


  • Washukiwa hao 13 walishtakiwa kwa makosa ya uhalifu kama vile kushambulia, ujambazi na wizi. 


Afisa wa polisi mlevi nchini Zambia amewaachilia washukiwa 13 kutoka kizuizini ili waende kusherehekea mwaka mpya, maafisa wanasema.

Inspekta wa upelelezi Titus Phiri alikamatwa baada ya kuwaachilia washukiwa hao kutoka kituo cha polisi cha Leonard Cheelo katika mji mkuu, Lusaka.

Washukiwa hao 13 walishtakiwa kwa makosa ya uhalifu kama vile kushambulia, ujambazi na wizi. Kwa sasa wote hawajapatikana na msako umeanzishwa ili kuwatafuta.

Afisa huyo alifungua gereza la wanaume na wanawake na kuwaagiza washukiwa waondoke huku akisema wako huru kusherehekea kuingia mwaka mpya.

Taarifa ya polisi inasema, kati ya washukiwa 15 waliokuwa kizuizini, 13 walitoroka, na baada ya tukio hilo, afisa huyo alikimbia eneo la tukio, kabla ya kukamatwa.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved