Wanamgambo wa Alshabab waliuawa katika operesheni iliyotekelezwa na wanajeshi wa nchi ya Somalia kwa ushirikiano na wanajeshi wa Marekani wa anga mnamo tarehe 5, Januari 2025.
Operesheni hiyo ilifanyika katika Kijiji cha Berhano, takriban kilomita 35 kutoka mji wa Kismayo. Vituo muhimu vya magaidi viliharibiwa wakati wa operesheni hiyo, na hakuna raia aliyejeruhiwa hii ni kutokana na ujumbe iliochapishwa kwenye mtandao ya X kupitia wizara ya habari, utamaduni na utalii nchini Somalia.
Jeshi la Marekani Jumatatu lilithibitisha kuuawa kwa kiongozi mkuu wa al-Shabab Mohamed Mire katika shambulio la anga la Desemba 24 karibu na mji wa Kunyo Barrow katika eneo la chini la Shabelle.
‘’Mnamo Desemba 24, kwa uratibu na ushirikiano na serikali ya shirikisho la Somalia, Amri ya jeshi la Marekani barani Afrika ilifanya shambulizi la anga la takriban kilomita 10 kusini magharibi mwa Quyno Barrow ambalo lilisababisha kifo cha kiongozi mkuu wa al-Shabaab, Mohamed Mire na mwanamgambo mwingine wa al-Shabaab,’’ Hii ni kutokana na mujibu wa U.S.Africa Command kupitia mtandao yao ya X.
Katika ujumbe yao amri ya jeshi la Marekani barani Afrika AFRICOM ilieleza kuwa Mire, anayejulikana pia kama Abu Abdirahman, aliwajibika kwa utawala wa kikanda wa al-Shabaab nchini Somalia kwa miaka 15 iliyopita. Mbali na kuwa mmoja wa wanachama waliokaa muda mrefu zaidi wa al-Shabaab, Mire aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na alichukua nafasi muhimu katika kufanya maamuzi ya kimkakati ya kundi hilo.
‘’Tutaendelea kutathmini matokeo ya operesheni hiyo na kutoa maelezo ya ziada kadri inavyofaa,” Alisema Jenerali wa jeshi la wanamaji la Marekani Michael Langley, kamanda wa AFRICOM, kulingana na taarifa hiyo.
AFRICOM ilisema haiwezi kufichua maelezo mahususi ya misheni hiyo, ikisema tu kwamba hakuna raia aliyejeruhiwa.
Al-Shabab, ambayo imekuwa ikipambana na serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 15, inadhibiti maeneo makubwa kusini mwa Somalia na kutawala eneo la kati la nchi hiyo na hata kushambulia nchi za jirani.