Chama cha wapiganiaji wa uhuru wa uchumi EFF cha Afrika Kusini kinachoongozwa na Julius Malema kimekubali kujiuzulu kwa wanachama wake wawili Yazini Tatyana na daktari Mbuyiseni Ndlozi kama wanachama wake katika uwakilishi kwenye bunge la kitaifa la nchi hiyo.
Julius Malema alikuwa kati ya wagombea wa urais wa Afrika Kusini katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana ila alipoteza na baadaye kuchaguliwa tena kama kiongzoi wa chama cha EFF mwezi Agosti mwaka jana.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari mapema Alhamisi asubuhi, cham cha EFF kimedhibitisha kupokea barua za kujiuzulu kwa waili hao na kimeridhia kuheshimu maombi yao ya kutaka kacha kuwa wawakilishi wa EFF kwenye bunge la Afrika Kusini.
Maombi ya kujiuzulu kwa Ndlozi na Tetyana yametwaja kuwa ya hiari kutoka kwa viongozi hao wawili.
EFF imetambua kwamba barua zilizowasilishwa kwa katibu mkuu wa EFF kutoka kwa Tetyana na Ndlozi mtawalia zilikuwa zimesheni shukrani kwa chama hicho kuwapa fursa za kuhudumia chama pamoja na wananchi wa Afrika Kusini.
EFF hata hivyo imekubali maombi ya wawakilishi hao ikiwashukurukwa mchango walioleta kwenye chama hicho.
“EFF imekubali maombi husika ya hiari ya kuachiliwa kutoka kwa kutumwa kwa wapiganaji hao wawili, ambao wametumikia shirika hili kwa bidii katika vikosi vyao kwa kuwa EFF imekuwa na uwakilishi katika nyanja ya kutunga sheria.” Sehemu ya taarifa ya EFF kwa vyombo vya habari iliarifu.
Kufikia kujiuzulu kwa viongozi hao, wamekuwa wakihudumu katika bunge la kitaifa la Afrika Kusini wakiwakilisha maeneo tofauti tofauti.
Mpiganaji Yazini Tetyana alikuwa akihudumu katika bunge la mkoa wa Cape mashariki sawia na bunge la Afrika Kusini.
Kwa upande mwingine mpiganiaji Mbuyiseni Ndlozi alikuwa
mwakilishi katika bunge la kitaifa kwa miaka kumi na zaidi kuanzia mwaka wa
2014.
EFF kilibuniwa mwaka wa 2013 na Julius Malema baada
ya kufurushwa kutoka kwa chama tawala cha Afrika Kusini African National
Congress (ANC).