Mkasa wa moto katika eneo la Los Angeles imeathiri watu
wengi hasa wale wa jumuiya ya Hollywood, wakiwemo Billy Crystal, Mandy Moore,
Jeff Bridges, Anna Faris na Ricki Lake miongoni mwa wengine wengi.
Mioto mikali huko Kusini mwa California imewalazimu wakazi zaidi ya 80,000 wa Los Angeles kuhama nyumba zao, wengi wao wameita eneo hilo nyumbani kwa miongo kadhaa wakiwemo baadhi ya nyota wakubwa wa Hollywood.
Janga hilo ilianza Jumanne 7, Januari 2025, asubuhi katika eneo la Pacific Palisades , na moto uliofuata ulizuka katika jamii za karibu kama vile Eaton na Woodley.
Crystal na mkewe, Janice, walitoa taarifa Jumatano wakisema kuwa nyumba yao ya miaka 45 katika kitongoji cha Pacific Palisades ilikuwa imeharibiwa kutokana na moto huo.
‘’Janice nami tuliishi nyumbani kwetu tangu 1979. Tulilea watoto na wajukuu wetu hapa. Kila inchi ya nyumba yetu ilijaa upendo. Kumbukumbu nzuri ambazo haziwezi kuondolewa, hakika tumeumia moyoni lakini kwa upendo wa watoto wetu na marafiki tutapitia haya,” Familia ya Crystal iliandika kwenye taarifa hiyo.
Mwigizaji na mtangazaji wa zamani wa kipindi cha mazungumzo kwa jina Lake alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Jumatano kwamba alipoteza "nyumba ya ndoto" kwenye moto huo, akamaliza kuandika kuwa, "Yote yamepita."
‘’Ilikuwa mbingu yetu hapa duniani. Mahali tulipopanga kuzeeka pamoja.hatukuwahi kuchukua nafasi yetu ya kimbingu kwa upuuzi unaongalia Malibu yetu mpendwa kwa urahisi, hata kwa sekunde moja,’’ Aliandika haya Lake.
Paris Hilton aligundua kuwa nyumba yake ya Malibu ilipotea wakati akiitazama ikiteketea kwenye televisheni ya moja kwa moja. Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram alisema kuwa picha hiyo ni kitu hakuna mtu anayepaswa kuona au kupitia.
Mpishi mashuhuri Sandra Lee pia alisema alipoteza nyumba yake kutokana na janga hilo la moto. Alikuwa alisema kuwa alisikitika na vitu zake za thamani zilizoungua katika nyumba yake.
“Nililia usiku kucha na kuwaza kuhusu kila chumba, chumba cha kulala na chumba cha kukula. Ilikuwa kamilifu na sasa ni jivu tu, Tafadhali waweke jumuiya yetu, wazima moto na waitikiaji wa kwanza katika maombi yako. Hii haijaisha na hata haikaribii kuisha bado." Aliandika Lee kwenye ukurasa wa Instagram.
Watu wengi mashuhuri wa hollyhood wanapitia wakati mgumu baada ya kugundua kwamba kitongoji chao cha matajiri cha Los Angeles kilibadilika kuwa majivu na vifusi wakati moto ulizuka Califonia na kusambaa palisades kote.
Idadi ya waliofariki kwenye moto huo wa kihistoria sasa imefikia 10, huku wazima moto mashujaa bado wanapambana na hali mbaya kwenye msatri wa mbele wa angalau moto tano tofauti.
Nyumba za Paris Hilton, Anthony Hopkins, Tina Knowles, John Goodman, Candy Spelling, Milo Ventimiglia, na Miles Teller ni miongoni mwa zilizoharibiwa, huku makumi ya nyota wengine sasa wanakabiliwa na kusubiri kwa wasiwasi pamoja na majirani zao ili kujua kama kuna baadhi ya vitu zao zilizookolewa.