logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Beyoncé atoa mchango wa dola milioni 2.5 kwa waathiriwa wa moto Los Angeles

Watu mashuhuri kama vile Tika Sumpter na Halle Berry wametoa bidhaa za kibinafsi , huku wengine wametoa usaidizi wa kifedha huku kukiwa na uharibifu wa mali nyingi eneo hilo

image
na OTIENO TONNY

Kimataifa13 January 2025 - 17:06

Muhtasari


  • Msaada huo unakuja baada ya Mkaguzi wa matibabu wa kaunti ya Los Angeles kuthibitisha kuwa idadi ya waliofariki kutokana na moto huo mbaya iliongezeka hadi watu 24 jumapili 12.
  • Licha ya kupoteza nyumba yake ya Malibu kwa moto, Paris Hilton alitoa mchango wa kibinafsi wa $ 100,000.


Beyoncé ametoa dola milioni $ 2.5  kusaidia jamii zilizoathiriwa na moto  unaoendelea kushuhudiwa Los Angeles. 

Siku ya Jumapili, Januari 12, taasisi ya mwimbaji ya BeyGOOD ilitangaza kupitia mtandao wa  Instagram kwamba Beyonce alitoa dola milioni $2.5  kwa hazina ya msaada wa moto ya Los Angeles  iliyoanzishwa na shirika lake la hisani.

‘’Tunasimama na nyinyi watu wa Los Angeles. Hazina hiyo imetengwa kwa ajili ya kusaidia familia katika eneo la Altadena/Pasadena waliopoteza makazi yao, na kwa makanisa na vituo vya jamii kushughulikia mahitaji ya haraka ya wale walioathiriwa na moto huo,” Hii ni kutokana na chapisho hilo kwa mtandao wa kijamii.

Aliwasihi watu kutembelea tovuti ya BeyGOOD ili kuonyesha msaada wao kwa familia zilizoathiriwa na pia kujifunza zaidi kuhusu taasisi yake ya kutoa misaada ya umma, ambayo alianzisha mwaka wa 2013.

Watu mashuhuri kama vile Tika Sumpter na Halle Berry wametoa bidhaa za kibinafsi , huku wengine wametoa usaidizi wa kifedha huku kukiwa na uharibifu wa mali nyingi eneo hilo.

Licha ya kupoteza nyumba yake ya Malibu kwa moto, Paris Hilton alitoa mchango wa kibinafsi wa $ 100,000 na akaahidi kuongeza na  dola za ziada zilizotolewa hadi  $ 100,000 zaidi kusaidia wengine wanaohitaji msaada zaidi.

Kwingineko Longoria alihisi hisia katika video katika mtandao wa Instagram akizungumzia uamuzi wake wa kutoa dola  $ 50,000 kwa shirika la ‘’This is About Humanity’’ kusaidia watu walioathiriwa na moto huo.

‘’Sidhani ni wakati wa kuchanganua kilichoharibika, Lazima tujaribu kumudu hali hiyo hivi sasa, kwa hivyo kila mtu ambaye yuko huko kusaidia na kufanya sehemu yake, asante sana,’’ Alisema Longoria.

Msaada huo unakuja baada ya Mkaguzi wa matibabu wa kaunti ya Los Angeles kuthibitisha kuwa idadi ya waliofariki kutokana na moto huo mbaya iliongezeka hadi watu 24 jumapili 12, Januari jioni.

Kulinganna na ripoti ya mkaguzi wa matibabu huyo, watu 16 kati ya watu waliouwawa kwenye moto huo walikuwa katika eneo la moto la Eaton wakati wengine wanane walipatikana karibu na eneo la Palisades.

Sherifu wa kaunti ya Los Angeles Robert Luna alifichua katika mkutano na wanahabari kwamba angalau watu 16 wameripotiwa kutoweka tangu mioto ya ajabu  ilipoanza Jumanne, Januari 7, kulingana na The New York Times.


 


 


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved