Rais mpya wa Marekani Donald Tramp ameiondoa marekani kutoka kwenye shirika linaloshughulikia maswala ya afyia ulimwenguni "WHO"
Tramp ambaye amechukua usukani hapo jana Januari 20 kuingoza marekani kwa miaka minne ijaayo, amesaini mabadiliko kadha katika serikali yake likiwemo hili la kuindoa marekani kutoka katika shirika la afia ulimwenguni. Tramp amerejea tena kwenyev ikulu ya White House miaka minne baada ya kutoka humo.
kwa mara ya kwanza Tramp aliongoza Marekani kati ya mwaka 2017-2021 kama rais wa 45 baada ya kuchukua usukani kutoka kwa mtangulizi wake Barack Obama wa chama cha Democrat.
kweye uchaguzi wa 2021 Trump alipototeza kiti hicho cha Urais kwa mpinzani wake Joe Byden, hivyo byden akamng'oa Trump mamlakani pamoja na chama chake cha Republican.
Katika uchaguzi wa mwaka jana 2024 Trump alijitosa tena uwanjani kuwania nafasi hiyo ya juu zaidi katika taifa la Marekani akimenyana na mpinzani wake wa chama ya Democrat Kamala Harris na akatua ushindi huo kama Rais wa 47. Zamu hii akipata umaarufu ulinganishwa na uchaguzi wa kwanza.
Donald Trump ameingia katika historia ya Marekani kama rais wa pili kuiongoza Marekani katika mihula miwili tofauti, akitoka na kurejea tena kwa mara ya pili.
Rais wa kwanza kuongoza hivyo alikua Grover Cleveland, rais wa 22 na 24 akiongoza kati ya mwaka 1885-1889 na akarejea tena 1893-1897.
Rais Trump kuiondoa Marekani kutoka katika shirika la afia ulimwenguni, huenda likawa pigo na kuhujumu juhudi za shirika hili.
Marekani ni mojawapo ya taifa lililokua linanachangia pakubwa zaidi katika shirika hilo maana taifa hilo lilikua likisimama kama viongozi wa shirika hilo la kupigania uhai na vile vile kutoa msaada wa matibabu hasa dawa kwa mataifa yasiyojiweza.
Shirika la afia ulimwenguni 'WHO' lilibuniwa mwaka 1948, na Marekani imekuweko tangu mwanzo wakishikilia wadhifa muhimu.
Baadhi ya malengo ya shirika hili ni pamoja na kupigana na magonjwa yanayosambaa kwa kasi, kufanya utafiti kwa changamoto zinazoathiri afia pamoja na jinsi ya kufikia matibabu kwa njia nzuri kwa mataifa yote.