Miili ya watu ipatao 93 imegunduliwa kwenye makaburi nchini Libya wakati wa uchunguzi kuhusu njia za uhamiaji wa binadamu, hili ni kulingana na umoja wa mataifa.
Kaburi la kwanza la watu wengi lilipatikana Feburuary 7 katika shamba la Jakharrah kasikazini mashariki mwa nchi ya Libya na siku moja baadaye kaburi lingine likagunduliwa eneo la Kufra kusini mashariki mwa nchi hio.
Kufikia sasa miili 93 imepatikana alivyoeleza katibu wa umoja wa mataifa anayeshughulikia maswala ya Afrika Rosemary DiCarlo wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama.
Siku kumi zilizopita mamlaka ya Libya ilisema kwamba iligundua miili 28 ya wahamiaji wa Sub- Saharan eneo la Kufra karibu na sehemu ambayo inadaiwa walikuwa wakifungiwa na Kuteswa.
Mamlaka ya nchi hiyo iliendelea kusema kwamba kaburi hilo liligunduliwsa baada ya uchunguzi katika eneo ambako biashara haramu ya binadam,u ilikuwa ikiendelea . Mamlaka ilisema kwamba iliwaachilia huru wahamiaji 76 kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara.
Uchunguzi huo ulilenga makundi ambalo yalinyimwa uhuru wao wa uhamiaji kimakusudi na waliteswa na na kunyanyaswa na kupitilizwa kwa vitendo visivyo vya kibinadamu," ofisi ya mwanasheria mkuu wa Libya ilisema tarehe tisa Feburuari.
Umoja wa Mataifa unaoshughulikia maswala ya uhamiaji nayo ikaripoti kaburi la pili la watu wengi upande wa Jakharrah.
" Kugunduliwa kwa makaburi ya watu wengi kunashitua na kunashangaza zaidi, hili linaweka wazi masaibu ambayo wahamiaji wanaotoroka makwao hukumbana nayo katika nchi ya Libya," alisema DiCarlo.
Libya ni nchi muhimu ya wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya, imejikakamua ili kujikwamua kutoka kwenye machafuko yaliyofuatia uasi wa mwaka 2011 ulioungwa mkono na NATO uliompindua dikteta wa muda mrefu Moamer Kadhafi.
Libya bado imegawanyika kati ya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa na mamlaka hasimu mashariki inayoungwa mkono na kiongozi wa kijeshi khalifa Hafter.
Walanguzi wa biashara haramu ya binadamu wamekuwa wakitumia fursa hiyo ya kutokuwa na utulivu nchini humo tangu zamani kuendeleza vitendo viovu hasa mauwaji ya kiholela pasipo sabau au hata kosa.