logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vifo kutokana na tetemeko la Myanmar vyafikia 2000, uokoaji ukiendelea

Mandalay iilipigwa na tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.7 siku ya Ijumaa ambalo lilisababisha uharibifu mkubwa nchini Myanmar

image
na BBC NEWS

Kimataifa31 March 2025 - 10:52

Muhtasari


  • Waokoaji wamemuokoa mwanamke mmoja aliyefunikwa na kifusi kwenye jango la hoteli moja lililoporomoka nchini Myanmar,
  • Gavana wa Bangkok, Chadchart Sittipunt alisema waokoaji hawakati tamaa.

Waokoaji

Waokoaji wamemuokoa mwanamke mmoja aliyefunikwa na kifusi kwenye jango la hoteli moja lililoporomoka nchini Myanmar, maafisa walisema siku ya Jumatatu..

Mwanamke huyo amekaa siku tatu baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha vifo vya watu 2,000 huku waokoaji nchini Myanmar na Thailand wakiendeslea kutafuta manusura zaidi.

Mwanamke huyo alitolewa kwenye vifusi baada ya saa 60 kukwama chini ya Hoteli ya Great Wall iliyoporomoka katika jiji la Mandalay baada ya operesheni ya saa 5 ya timu za waokoaji kutoka China, Urusi na wenyeji, kulingana na chapisho la ubalozi wa China kwenye Facebook. Ilisema alikuwa katika hali nzuri mapema Jumatatu.

Mandalay iilipigwa na tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.7 siku ya Ijumaa ambalo lilisababisha uharibifu mkubwa nchini Myanmar na uharibifu katika nchi jirani ya Thailand.

Huko Bangkok, mji mkuu wa Thailand, wafanyakazi wa dharura wanaotumia mbwa siku ya Jumatatu waliendelea na msako mkali wa kuwatafuta watu 76 wanaoaminika kufukiwa chini ya vifusi vya jumba kubwa lililoporomoka.

Gavana wa Bangkok, Chadchart Sittipunt alisema waokoaji hawakati tamaa.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved