Jamaa anayedaiwa kuwa mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Japan azungumza

Kojima ametishia kuwashtaki wanaoeneza uvumi kuwa yeye ndiye muuaji wa Shinzo Abe.

Muhtasari

•Hideo Kojima amehusishwa na kupigwa risasi kwa waziri mkuu wa zamani wa Japan na picha zake zimewekwa kwenye tovuti mbalimbali.

Image: BBC

Mtengenezaji maarufu wa michezo ya sauti na video ametishia kuwashtaki wanaoeneza uvumi wa uongo kuwa yeye ndiye muuaji wa Shinzo Abe.

Hideo Kojima, mvumbuzi na mbunifu wa mchezo wa ‘’Metal Gear’’ amehusishwa na kupigwa risasi kwa waziri mkuu wa zamani wa Japan, na picha zake zimewekwa kwenye tovuti ya 4chan.

Picha hizo zilifuatiwa na mwanasiasa wa Ufaransa, na pia ziliripotiwa na vyombo vya habari nchini Ugiriki na Iran.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na fundi huyo, Kojima Productions, ilisema analaani vikali kuchapishwa kwa habari hizo za uongo.

Tovuti ya 4chan ilitumia picha ya Kojima na kwa uwongo ilidai kuwa ‘’mrengo wa kushoto mwenye msimamo mkali’’ na aliwahi kufanya uhalifu hapo awali.

Vyombo vya habari pia viliripoti picha nyingine inayoonyesha kofia ya chuma iliyovaliwa na wanajeshi wa Urusi na nyingine iliyosimama karibu na picha ya Che Guevara, mwanaharakati mwenye itikadi kali.