logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mabaki ya mtoto wa miaka 8 yapatikana kwenye tumbo la mamba

Mtoto huyo alikuwa anacheza kando ya mto kabla ya mamba kumvamia.

image
na Radio Jambo

Kimataifa01 December 2022 - 09:25

Muhtasari


•Wanafamilia walikuwa wakicheza karibu na ufuo wa mto wakati mnyama huyo alipomrukia na kumshambulia.

• Wakaazi walimvamia mamba huyo, wakamuua na hatimaye kumpasua tumbo na kuyatoa mabaki ya mwili wa mtoto.

Mamba mkubwa

Mabaki ya mtoto wa miaka 8 ambaye alimezwa na mamba akiwa hai yalipatikana tumboni mwa mnyama huyo.

Wakaazi wa kijiji kimoja cha Costa Rica walikumbwa na huzuni nyingi wakati mabaki ya mtoto huyo yaliltolewa siku mbili baada ya kumezwa na mamba huyo.

Vituo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti kuwa kijana huyo Julio Otero pamoja na baadhi ya wanafamilia walikuwa wakicheza karibu na ufuo wa mto wakati mnyama huyo alipomrukia na kumshambulia.

Mama yake ambaye alifanya kasi kujaribu kumsaidia huku akipiga kamsa alikuwa karibu kuumwa pia. Juhudi zake hata hivyo ziliangulia patupu kwani mwanawe aliburutwa na mamba huyo na kutoweka.

Timu ya uokoaji ya msalaba mwekundu kwa ushirikiano na polisi walifanya juu chii kumtafuta mamba huyo kwa siku mbili mtawalia bila mafanikio. Wanakijiji ambao walikuwa na dhamira kubwa ya kumnasa mnyama huyo walimtafuta kwa udi na uvumba hadi hatimaye juhudi zao zikazaa matunda.

Kabla ya polisi kufika katika eneo hilo, tayari wakaazi waliojawa na hamaki walikuwa wamemvamia mamba huyo, wakamuua na hatimaye kumpasua tumbo na kuyatoa mabaki ya mwili wa mtoto.

Mama mtoto ambaye alishuhudia mwanawe akivamiwa, alibainisha kuwa mabaki hayo ni ya Otero . Polisi walichukua nywele na mifupa na kufanya uchunguzi ili kubaini kama mabaki ni mtoto huyo mdogo.

Uchunguzi uliweza kubaini kuwa mifupa hiyo ilikuwa ya Otero.

Mabaki ya mtoto yapatikana kwenye tumbo la mamba


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved