Mchungaji taabani baada ya kumlipa muuaji 5.3m ili kumpiga risasi mpenzi wa bintiye

Mshukiwa alishtakiwa kwa kulipia mauaji, kula njama ya mauaji, kujaribu kuua na kushambulia kwa silaha mbaya.

Muhtasari

•Mchungaji Samuel Pasilla alishtakiwa kwa kuwalipa wauaji karibu Sh5.3m ili kumpiga risasi mpenzi wa bintiye.

•Mlengwa alijiendesha mwenyewe hadi hospitalini akiwa na majeraha ya risasi na kuripoti kuwa alishambuliwa.

Image: Maktaba// rozali

Mchungaji mmoja mwenye umri wa miaka 47 kutoka California, Marekani yuko matatani baada ya kushtakiwa kwa kuwalipa wauaji karibu dola 40,000 (Sh5.3m) ili kumpiga risasi mpenzi wa bintiye.

Mchungaji, Samuel Pasilla alikuwa mmoja wa wanaume wawili waliokamatwa kuhusiana na uchunguzi wa mauaji ya kulipwa ulioanza mwaka jana baada ya jaribio lililotokea Riverside. Mlengwa hata hivyo hakuuawa katika shambulio hilo ila alijeruhiwa.

Katika taarifa ya Jumanne Idara ya Polisi ya Riverside ilisema Bw. Pasillas alikamatwa mnamo Machi 13 na kushtakiwa kwa kulipia mauaji, kula njama ya mauaji, kujaribu kuua na kushambulia kwa silaha mbaya.

Juan Manuel Cebreros, 55, pia alikamatwa kwa tuhuma za kula njama ya mauaji, kujaribu kuua na kushambulia kwa silaha mbaya.

Polisi hawakumtambua mara moja mshukiwa mwingine yeyote.

Uchunguzi huo ulitokana na tukio la kupigwa risasi Oktoba 21, wakati mwanamume mmoja alipojiendesha mwenyewe hadi hospitalini akiwa na majeraha ya risasi na kuripoti kuwa alishambuliwa alipokuwa akiendesha gari mwendo wa saa moja usiku.

Jamaa aliyepigwa risasi, ambaye hakutambuliwa na mamlaka, alisema gari lingine lilisimama kando yake alipokuwa akikaribia mtaa wa Plainview.

Kisha, risasi zilianza kupigwa.

Kufuatia uchunguzi wa kina, wapelelezi waligundua kwamba shambulio hilo lilikuwa la uuwaji wa risasi.

 Mwanamume ambaye alilengwa alikuwa akichumbiana na mwanamke ambaye baba yake ni mchungaji katika kanisa moja katika jiji la Victorville. Taarifa hiyo ya polisi ilimtaja Bw.Pasillas kuwa ndiye mchungaji.

Wapelelezi walipata ushahidi kwamba Bw. Pasillas alikutana na wanaume aliowalipa na kuwapa taarifa kuhusu mlengwa, ikiwa ni pamoja na mahali ambapo angekuwa jioni ya kupigwa risasi.

Polisi  walisema kuwa Bw. Pasillas alilipa karibu dola 40,000 na kwamba alikuwa amemchunguza mwathiriwa katika wiki chache kabla ya kupigwa risasi.

Washukiwa walikamatwa Machi 13 kufuatia uchunguzi.

Bw. Pasillas na Bw. Cebreros walishikiliwa na kupewa bondi za dola milioni 1..Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Machi 26.