Seneta Murkomen asherehekea BBI kuaguka

Muhtasari

• meshikilia kwamba BBI haikufuata sheria a hivyo ilipaswa kuangushwa.

• "Haikuwa sawa kisheria, narudia haikuwa sawa kisheria," Murkomen aliandika.

Seneta wa kaunti ya Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen ameonyesha furaha yake baada ya mswada wa BBI kutupiliwa mbali na mahakama ya upeo.

Kupitia ujumbe alioandika katika ukurasa wake wa Facebook, Murkomen alisema kwamba mswada huo haustahiki kabisa kuidhinishwa na unapaswa kukataliwa kwa hali hali zote.

"Haikuwa sawa kisheria, narudia haikuwa sawa kisheria," Murkomen aliandika.

Murkome ni moja kati ya viongozi waliopo katika chama cha UDA ambao wamekuwa wakipinga vikali kuidhinishwa kwa mswada huo wa BBI kuwa sheria.

Viongozi waaogemea upande wa naibu rais William Ruto, walikuwa wakipinga mchakato huo wa kuifanyia katiba marekebisho kwa kile walikitaja kuwa, mswada huo ulikuwa unalenga kuwanufaisha viongozi wachache serikali na kuwaacha wananchi wakihangaika.

Kupitia kwa jaji mkuu Martha Koome, mahakama ya upeo ilisema kwamba rais Uhuru Kenyatta hakuwa na uwezo kisheria kuasisi mchakato wa kuifanyia katiba mabadiliko.