Mwanamume akanusha kughushi hati za korti

Muhtasari
  • Mwanamume akanusha kughushi hati za korti
  • Mshtakiwa alikana mashtaka yote mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa Milimani Bernard Ochoi na kuomba kuachiliwa kwa dhamana
Mahakama ya Milimani mjini Nairobi
Mahakama ya Milimani mjini Nairobi

Mwanamume mmoja ameshtakiwa kwa kutengeneza hati ya korti na kutoa ushahidi wa uongo mbele ya mahakama.

George Thiongo Mathu alishtakiwa kwa makosa kadhaa yakiwemo ya uongo na kutengeneza hati bila mamlaka.

Hati ya mashtaka ilieleza kuwa alikula njama ya kutenda kosa kwa kughushi na kusaini kesi mahakamani, notisi ya Hoja katika CMCC NSo.6364 ya mwaka 2014, akidai kuwa imechorwa na kusainiwa na Nguji B.G & Company AdvocateS.

Mahakama ilisikiliza kwamba alitenda kosa hilo, kwa pamoja na wengine ambao tayari wamefunguliwa mashtaka, Oktoba 22, 2014.

Mahakama ilisikiza zaidi kwamba mnamo Oktoba 23, 2014, alitoa ushahidi katika mahakama ya kibiashara ya Milimani jijini Nairobi katika kesi ambapo Ernest S. Kamau Nduati aliishtaki Kampuni ya Henkam Company Ltd.

Mwendesha mashtaka alisema kwa kujua alitoa ushahidi wa uongo kugusa jambo husika.

Kesi hiyo ilikuwa ya kutaka malipo ya Sh6 milioni kama tume ya mauzo ya Hoteli ya Princess. Mahakama ilisikia alidai kuwa ameidhinishwa, mashirika yaliyoruhusiwa na yenye kandarasi kupata mnunuzi.

Mshtakiwa alikana mashtaka yote mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa Milimani Bernard Ochoi na kuomba kuachiliwa kwa dhamana.

Aliachiliwa kwa bondi ya Sh 500,000. Kesi hiyo itatajwa baada ya wiki mbili.