Mshukiwa wa mauaji ya Muvota ashikiliwa kwa siku 14

Muhtasari
  • Afisa huyo aliambia Mahakama kwamba alihitaji siku 14 ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi
  • Mtuhumiwa huyo anadaiwa kukutwa eneo la tukio na upelelezi unaendelea kuhusu mauaji ya Muvota
Mshukiwa wa mauaji ya mfanyibiashara Muvota,Dennis Karani
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mwanamume anayeshukiwa kutekeleza mauaji ya mfanyabiashara tata katika Barabara ya Mirema Nairobi amezuiliwa kwa siku 14 akisubiri uchunguzi.

Katika maombi tofauti yaliyowasilishwa mahakamani na afisa mchunguzi Kapario Lekakeny, inadai kuwa Dennis Karani ndiye aliyekuwa dereva wa gari lililotumiwa katika eneo la mauaji ya Samuel Mugo Muvota.

Afisa huyo aliambia Mahakama kwamba alihitaji siku 14 ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kukutwa eneo la tukio na upelelezi unaendelea kuhusu mauaji ya Muvota.

"Naiomba mahakama kuchukua taarifa ya video hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mwanamume mmoja alinaswa na kamera za CCTV. Ili kuondoa mashaka uhalifu huo ulifanywa na zaidi ya watu wawili kwani inaonekana aliyebadilisha mauaji hayo kwa gari lililokuwa limeegeshwa", mahakama iliambiwa.

Karani anashukiwa kuwa nyuma ya usukani.

Anashukiwa kuwa na bunduki.

"Tunahitaji siku 14 ambazo zinatosha na tunahitaji kusafiri hadi Mombasa, Nakuru na Kiambu ambako inaaminika mshukiwa ana nyumba na bunduki iko ndani", Lekakeny alisema.

Mshukiwa aliiambia mahakama kuwa hana pingamizi na upelelezi na akasema yuko tayari kwa upelelezi.

Karani alifikishwa mbele ya hakimu mkazi mkuu wa Milimani Caroline Muthoni na kuruhusu polisi kumzuilia Karani katika kituo cha polisi cha Kasarani kwa siku 14. Kesi hiyo itatajwa Juni 8.

Dennis alijisalimisha mikononi mwa polisi mnamo siku ya Jumatatu.

Dennis Karani Gachoki alidai hana hatia na alikutana na Muvota mara mbili pekee, mara moja Meru na Nairobi.

Alijisalimisha kwa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai makao makuu akiwa ameambatana na wakili.