Maafisa wa mahakama wazuru eneo la mauaji ya Monica Kimani

Muhtasari

•Inspekta Mkuu Maxwell Otieno aliambia mahakama kuwa Jowie alifika kwa gari la abiria na kutumia kitambulisho kilichoibwa kuingia bomani.

•Hakimu, mshtakiwa na mawakili walitembelea nyumba hiyo lakini hawakupita mlangoni kwa sababu kuna mpangaji mpya

Bustani ya Lamuria ambapo Monica Kimani aliwahi kukaa kwenye kesi ya Jowie na Maribe.
Bustani ya Lamuria ambapo Monica Kimani aliwahi kukaa kwenye kesi ya Jowie na Maribe.
Image: ANNETTE WAMBULWA

Mahakama inayosikiliza kesi ya Jacque Maribe na Joseph Irungu ambao wamehusishwa na mauaji ya Monica Kimani Jumatano ilitembelea Lamuria Gardens katika eneo la Kilimani, Nairobi, ambapo  aliuawa. 

Jaji Grace Nzioka alionyeshwa lango ambalo Jowie anadaiwa kutumia kuingia kwenye nyumba hiyo. 

Inspekta Mkuu Maxwell Otieno aliambia mahakama kuwa Jowie alifika kwa gari la abiria na kutumia kitambulisho kilichoibwa kuingia bomani.

Kulingana na Otieno, jinsi Jowie alivyoingia ndani ya boma hilo ilionyesha kwamba alipajua mahali hapo vyema huku akitembea moja kwa moja hadi nyumbani kwa Monica. 

Hakimu, mshtakiwa na mawakili walitembelea nyumba hiyo lakini hawakupita mlangoni kwa sababu kuna mpangaji mpya ambaye lazima usiri wake ulindwe. 

Kutoka Lumuria Gardens, mahakama itaelekea katika eneo la Hurlingam na kutembelea Communication Centre, nje ya Barabara ya Dennis Pritt ambapo Citizen TV ipo. 

Akiwa langoni, wakili Katwa Kigen ataonyesha korti jinsi data ya simu ya Maribe ilinaswa Lamuria.

 Anatazamia kuonyesha umbali kati ya Lamuria na Mwananchi na jinsi data yake huenda ilinaswa. 

Wakati huo huo, Otieno ameambia mahakama kwamba Jowie alikuwa Roadhouse Grill jioni ya mauaji hayo kutoka ambapo wanaamini alienda kwa nyumba ya Monica. 

Alisema Roadhouse Grill iko umbali wa mita 100 kutoka Bustani ya Lamuria.  Afisa wa uchunguzi alisema kabla ya Jowie kwenda Lamuria, alibadilika na kuwa Kanzu (vazi la kidini la Kiislamu).

Otieno alisema Jowie alikuwa akiendeshwa kwa gari la Maribe kutoka Roadhouse Grill. 

Aliambia mahakama kwamba hakukuwa na picha za CCTV kuanzia siku hiyo.