Habari za hivi sasa! Mahakama ya juu yamtoa Sonko kinyang'nyironi

Juzi mahakama kuu ilitoa uamuzi wa kutaka IEBC kumruhusu kuwania kama gavana Mombasa

Muhtasari

• Habari za hivi sasa! Mahakama ya juu yamtoa Sonko kinyang'nyironi 

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko
Image: Facebook// Mike Sonko

Habari za hivi sasa! Mahakama ya juu yamtoa Sonko kinyang'nyironi 

Safari ya Sonko kutafuta  ugavana wa Mombasa huenda imetiwa kikomo baada ya mahakama ya Juu siku ya Ijumaa kutupilia mbali rufaa yake.

Mahakama hiyo ilishikilia maamuzi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa, ikithibitisha kuondolewa kwa aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko.

Katika uamuzi huo, mahakama kuu ilikubaliana na maamuzi ya mahakama ya chini ya kuunga mkono kuondolewa kwake afisini na Seneti.

Majaji saba wakiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome walisema walitupilia mbali rufaa ya Sonko kwa kukosa mamlaka ya kushughulikia swala hilo.

Mahakama ya Juu ilisikiliza rufaa hiyo ambapo pande zote zilipinga kesi zao huku Sonko akisisitiza kuwa kuondolewa kwake hakukuafikia vigezo vilivyowekwa chini ya Katiba.

Rufaa hiyo ilisikizwa siku moja tu baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)kumuidhinisha kuwania kiti cha Gavana wa Mombasa katika uchaguzi wa Agosti.

Mnamo Desemba 3, 2020, Sonko alitimuliwa na Wakilishi wadi 88 wa Bunge la Kaunti ya Nairobi.

Kesi hiyo baadaye ilipelekwa kwa Seneti, kama inavyotakiwa na Katiba mnamo Desemba 17, 2020, ambapo waliidhinisha azimio la kumwondoa afisini.