Omanyala atetea Wizara ya michezo kuhusu maandalizi ya mashindano ya Uregon

Uchunguzi huo unajiri kufuatia madai ya kujumuishwa kwa watu 32 kwenye orodha ya wanariadha.

Muhtasari

• Taarifa iliyotolewa Ijumaa, polisi waliomba Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kutoa nakili za Kamati ya Kitaifa ya usimamizi wa riadha.

 

Mwanariadha wa Timu ya Kenya baada ya kuwasili kutoka kwa michuano ya Afrika nchini Mauritius. Picha: PSCU
Mwanariadha wa Timu ya Kenya baada ya kuwasili kutoka kwa michuano ya Afrika nchini Mauritius. Picha: PSCU

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu usimamizi wa wanariadha walioshiriki mashindano ya riadha ya dunia huko Oregon.

 

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, polisi waliomba Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kutoa nakili za Kamati ya Kitaifa ya usimamizi wa riadha.

 

“Ili kurahisisha uchunguzi wetu, tunahitaji makadirio ya bajeti, na mchanganuo wa malipo yote na vocha za malipo za wanariadha wote na maofisa wakuu  walioshiriki katika maandalizi wa mashindano hayo,” ilisema taarifa hiyo.

 

Polisi pia watahitaji ombi la ununuzi na uidhinishaji wa tikiti za ndege, orodha ya wanariadha wote waliohitimu katika kila fani na barua kutoka kwa Chama cha riadha nchini (AK) kuonyeshs ombi la kuezesha  upatikananji wa visa na tikiti za ndege.

 

Haya yanajiri baada ya Ferdinand Omanyala nusura akose kufika kwa wakati kushiki mchujo wa mita 100 mjini Oregon kutokana na kucheleweshwa kwa visa.

 

Ucheleweshaji huo ulilaumiwa kwa Omanyala kutofika kwa muda uliotakikana.

 

Omanyala alipokea visa hiyo muhimu kufuatia kelele  kutoka kwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii waliokashifu Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi kwa kuchelewa kumpa bira.

 

Uchunguzi huo unajiri kufuatia madai ya kujumuishwa kwa watu 32 kwenye orodha ya wanariadha.