Mvulama 16, afikishwa mahakamani kwa kumnajisi msichana 12

Mamake msichana aliambia mahakama jinsi bintiye alikuja nyumbani akivuja damu

Muhtasari

• Kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha Polisi cha Loitoktok ambapo msichana huyo alisindikizwa katika hospitali ndogo ya Loitoktok kwa matibabu.  

• Baadaye mshtakiwa alikamatwa na hatimaye kushtakiwa kwa kosa la dhulma za kimapenzi madai ambayo alikana.

Mahakama
Mahakama

Mvulana mmoja mchungaji wa ng’ombe mwenye umri wa miaka 16 siku ya Jumanne alifikishwa mbele ya mahakama ya Loitoktok kushtakiwa kwa kumnajisi msichana wa miaka 12.

Kijana huyo aliyefikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Judicaster Nthuku anadaiwa kumnajisi mtoto huyo Januari 22, mwaka huu katika eneo la Nchalai, Kaunti Ndogo ya Loitoktok.

Akitoa ushahidi wake, msichana huyo aliambia mahakama kwamba siku hiyo yeye na kakake mwenye umri wa miaka 6 walikuwa wameenda kuchunga ng'ombe wao mbali na nyumbani.

Msichana huyo alisimulia jinsi kakake akienda kuangalia ng’ombe kwa mbali, mshtakiwa aliibuka msituni na kumfinyia chini na kumnajisi huku akipiga mayowe ili kuomba msaada.

Alisema mayowe hayo yalimfikia kakake ambaye alikuja na kumkuta akivuja damu na kumwambia aende nyumbani.

Mamake Mary Naboru aliambia mahakama jinsi bintiye alitoka malishoni akivuja damu na kumsimulia masaibu aliyopitia.

Kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha Polisi cha Loitoktok ambapo msichana huyo alisindikizwa katika hospitali ndogo ya Loitoktok kwa matibabu.  

Baadaye mshtakiwa alikamatwa na hatimaye kushtakiwa kwa kosa la dhulma za kimapenzi madai ambayo alikana.             

Katika utetezi wake kijana huyo alisema hamjui mlalamishi akishikilia kuwa hana hatia. Hukumu itatolewa Alhamisi ijayo.

TAFSIRI: DAVIS OJIAMBO.