Mahakama ya upeo imesema si jukumu lake kusuluhisha ni wakili gani atakayewakilisha IEBC katika Mahakama ya Juu.
Katika uamuzi wake Jumanne, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu alisema mzozo kati ya makamishna ni wa ndani.
"Mahakama hii haiwezi kushughulikia suala au mzozo wa uwakilishi wa kisheria wa IEBC katika ombi hili," alisema.
"Tumezingatia shauri. Sio shughuli ya mahakama bali ni suala la ndani ambalo lazima lisuluhishwe na IEBC na makamishna. Mahakama hii haitoweza. kuingizwa kwenye mzozo huu."
Mwilu alisema makamishna hao wanne wanaweza kutumia huduma za Paul Muite kama wataona ni muhimu katika shughuli hiyo.