IEBC:Tumeipa Azimio idhini ya kufikia seva

, Jaji Isaac Lenaola alisema kuwa IEBC inafaa kuwapa walalamishi "uwezo unaosimamiwa ambao sio wa kusoma pekee"

Muhtasari
  • Hapo awali alipokuwa akitoa wasilisho lake, wakili mkuu James Orengo alidai walikuwa wamepewa idhini ya kufikia seva moja pekee tofauti na nane
akizungumza katika Bomas of Kenya mnamo Agosti 9, 2022
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati akizungumza katika Bomas of Kenya mnamo Agosti 9, 2022
Image: ENOS TECHE

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka imeidhinisha Azimio ufikiaji wa kisheria kwa seva zao.

Tume hiyo ilitoa tangazo hilo kwenye mitandao ya kijamii Jumatano kufuatia maagizo yaliyotolewa Jumanne na Mahakama ya upeo.

"Kufuatia agizo la Mahakama ya upeo, IEBC imeruhusu wahusika kupata seva na uchunguzi unaendelea," tume hiyo ilisema kwenye Twitter.

Hapo awali alipokuwa akitoa wasilisho lake, wakili mkuu James Orengo alidai walikuwa wamepewa idhini ya kufikia seva moja pekee tofauti na nane.

"Tumepewa ufikiaji mdogo tu kwa matokeo yanayotumwa. Na bado tunaelewa kuwa IEBC ina seva nane," Orengo aliambia mahakama.

Alipokuwa akitoa maagizo kuhusu ufikiaji wa seva mnamo Jumanne, Jaji Isaac Lenaola alisema kuwa IEBC inafaa kuwapa walalamishi "uwezo unaosimamiwa ambao sio wa kusoma pekee" kwa seva zake katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha.

"IEBC italazimika kuwapa waombaji wanaosimamiwa idhini ya kufikia seva/seva zozote katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura ili kuhifadhi na kusambaza taarifa za upigaji kura na ambazo zina taswira ya kitaalamu ili kunasa nakala ya Fomu 34C ambayo ni jumla ya kura zilizopigwa."