logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kisumu: Mwalimu mkuu wa kiume afutwa kwa kuruhusu mwanafunzi wa kike kumpikia

Mwanafunzi huyo alipika chakula kwa mwalimu mkuu na kuondoka na baadhi ya chakula hicho kwenda bwenini.

image
na Davis Ojiambo

Habari06 November 2022 - 10:09

Muhtasari


  • • TSC ilimfuta mwalimu huyo bila kumpa takrima yoyote aliyokuwa amedai mahakamani.
  • • Sasa atakabidhiwa tu cheti cha kuhudumu kama mwalimu tangu mwaka 1990.
Mchoro wa mwanaume aliyesongwa na mawazo

Mahakama ya Kisumu imedumisha kufutwa kazi kwa mwalimu mmoja mkuu wa shule aliyemruhusu mwanafunzi wa kike kumpikia nyumbani kwake.

Mwalimu Mkuu wa shule, Gregory Onyango Obonyo, alikiri makossa kwa mwajiri wake TSC ya kumkubalia mwanafunzi wa kike ambaye alikuwa mgonjwa kupika chakula katika nyumba yake na hata kumpakulia baadhi ya chakula hicho kwenda nacho katika bweni lao.

Katika kile kilichoonekana kama kitendo cha wema kilichorudi na majibu tofauti, mwalimu huyo alidhibitishwa kufutwa kazi na hata ombi lake la kutaka apewe kiasi cha pesa kwa sababu ya kufutwa kwake kufutiliwa mbali.

“Sasa hana kazi - alifutwa kazi na Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) na kufukuzwa kwake kulithibitishwa na Mahakama ya Ajira na Mahusiano ya Kazi mnamo Oktoba 27. Pia, alikuwa amedai fidia ya Shilingi milioni 5.6, nyingi zikiwa takrima. Mahakama, iliyoko Kisumu, ilisema hatakiwi kulipwa senti kwa kushindwa kuthibitisha kwamba ana haki ya kupata takrima; na kwamba atapewa tu cheti cha utumishi,” jarida la Nation liliripoti.

Kazi ya mwalimu hiyo inafika kikomo kwa njia ya utata baada ya kuhudumu kama mwalimu tangu mwaka 1990.

Mahakama ilielezwa kuwa mwanafunzi huyo alipelekwa kwa mwalimu mkoo na walimu wa usimamizi wa bweni ambapo alieleza kuwa alikuwa mgonjwa na alikuwa amelala katika bweni kwa siku mzima.

Mwalimu huyo mkuu alimpa hifadhi katika nyumba yake na kuenda kumtafutia chakula ambacho alimuagiza kukipikia hapo ndani kwake baada ya kumpa dawa na kumruhusu kuondoka kuelekea bwenini na baadhi ya chakula hicho alichopika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved