Aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa IEBC Oswago atozwa faini ya milioni 7.5 au kifungo cha miaka 4 jela

Mnamo 2013, Oswago na Wilson Shollei walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kukosa kufuata sheria inayohusiana na ununuzi.

Muhtasari
  • Wawili hao wanadaiwa kukosa kuhakikisha mabadiliko yaliyofanywa kwa kandarasi iliyotolewa kwa Face Technologies Limited na IEBC
Mahakama
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa IEBC James Oswago amehukumiwa kulipa faini ya Sh7.5 milioni au kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kutoa zabuni ya Sh1.3 bilioni kinyume cha sheria kwa usambazaji wa nyenzo za wapiga kura katika uchaguzi Mkuu wa 2013.

Mshtakiwa mwenzake Wilson Shollei pia amepewa hukumu sawa.

Mnamo 2013, Oswago na Wilson Shollei walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kukosa kufuata sheria inayohusiana na ununuzi.

Wawili hao wanadaiwa kukosa kuhakikisha mabadiliko yaliyofanywa kwa kandarasi iliyotolewa kwa Face Technologies Limited na IEBC kwa usambazaji wa Kitambulisho cha Kielektroniki cha Mpiga Kura katika Zabuni Nambari ya IEBC14/2011- 2012 ziliidhinishwa na kamati ya zabuni ya IEBC.

Katika shtaka tofauti, walishtakiwa kwa kutumia ofisi zao kutoa faida isivyofaa kwa Kampuni ya Face Technologies Limited kwa kuidhinisha malipo ya Sh1,397,724,925.51 kwa usambazaji wa EVIDs bila kuthibitisha kuwa vifaa vilivyotolewa vilikaguliwa, kukubaliwa na kutimiza masharti ya kiufundi mkataba.